Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema kwamba watasajili wachezaji watatu zaidi baada ya kipa Juma Kaseja na lengo lao ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa mwakani.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Bin Kleb alisema baada ya kufanikisha usajili wa kipa Juma Kaseja, sasa wanahamia katika nafasi nyingine kuboresha timu yao.
Alisema watasajili beki mmoja wa kati, kiungo mkabaji na mshambuliaji mmoja ambao hata hivyo alisema bado mchakato wa kuwatafuta unaendelea.
“Tunataka kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa mwakani, tunahitaji kuandaa timu vizuri pamoja na kusajili. Tatizo kubwa ni kalenda hii imekaa vibaya, kiasi kwamba tunakosa muda wa kuiandaa timu vizuri,”.
“Mwezi huu wachezaji wetu wengi watakwenda Kenya na timu ya taifa kwenye michuano ya Challenge, wakirudi tu kuna mechi dhidi ya Simba ya Ngao ya Hisani Mwanza ambayo imeandaliwa na wadhami TBL,”
“Kwa hivyo unakuta muda wa mwalimu kutekeleza programu yake vizuri unakosekana, ila tutapambana na hali hiyo kwa vyovyote ili kutimiza malengo yetu,”alisema.

![]() |
| Bin Kleb akimsainisha Juma Kaseja mwishoni mwa wiki |

.png)
0 comments:
Post a Comment