• HABARI MPYA

    Wednesday, November 06, 2013

    AMISI ‘TAMBWE TEN’ OGOPA SANA STRIKER HUYU WA SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    AMISI Tambwe leo ameinua mikono miwili juu akiikunja mithili ya ngumi- baada ya kufunga bao la 10 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ashanti United na kuendelea kuongoza kwa mabao katika ligi hiyo.
    Alikuwa anamaanisha 10- yaani mabao 10 katika mechi 11 alizocheza msmu huu na sasa Mrundi huyo anamzidi kwa mabao mawili, Mganda Hamisi Kiiza wa Yanga mwenye mabao manane sawa na Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na Elias Maguri wa Ruvu Shooting.
    Salamu kwa Kiiza; Amisi Tambwe akionyesha ngumi mbili kumaanisha mabao 10 aliyofikisha leo 

    Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche wa Azam FC, raia wa Ivory Coast ana mabao saba sawa na Themi Felix wa Kagera Sugar, wakati Mrisho Ngassa ana mabao matano sawa na Didier Kavumbangu anayecheza naye Yanga SC na Tumba Swedi wa Ashanti United, ambaye ndiye beki mwenye mabao mengi zaidi msimu huu hadi sasa.
    Kiiza na Kipre Tchetche wana nafasi za kuongeza mabao watakapokuwa wakizichezea timu zao kesho mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Yanga ikimenyana na JKT Oljoro na Azam FC na Mbeya City. 

    WAFUNGAJI WA MABAO LIGI KUU:
    JINA TIMU MABAO
    Amisi Tambwe Simba SC 10
    Hamisi Kiiza Yanga SC 8
    Juma Luizio Mtibwa 8
    Elias Maguri Ruvu Shoot 8
    Kipre Tchetche Azam FC 7
    Themi Felix Kagera 7
    Mrisho Ngassa Yanga SC 5
    Tumba Swedi Ashanti 5
    D. Kavumbangu Yanga SC 5
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMISI ‘TAMBWE TEN’ OGOPA SANA STRIKER HUYU WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top