• HABARI MPYA

    Wednesday, October 30, 2013

    WENGER NI KIBONDE WA MILELE WA JOSE MOURINHO, HAKUNA UBISHI

    USIJALI sana Arsene – bila shaka itakuwa bahati ya mara ya 10 wakati Jose Mourinho na timu yake, Chelsea watakapokwenda Uwanja wa Emirates Jumatatu ya Desemba 23, mwaka huu.
    Kipigo cha Arsenal cha mabao 2-0 katika Kombe la Ligi maarufu kama Capital One kutoka kwa Chelsea usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tisa Wenger anakutana na Mourinho na kutoka kichwa chini.
    Rekodi yake dhidi ya Mreno huyo inamaanisha yeye ni mnyonge: amefungwa mara tano na kutoa sare nne. Anapotokea Mourinho, Wenger ni kibonde sana.
    Ubabe pale pale: Ushindi wa Chelsea kwa Arsenal unamfanya Jose Mourinho aendeleze rekodi ya kutofungwa na Arsenal Wenger (chini)

    Arsenal manager Arsene Wenger watches the League Cup fourth round match against Chelsea
    Old foes: Mourinho and Wenger greet each other before the Capital One Cup clash
    Mourinho na Wenger walisalimiana kabla ya mechi ya Kombe la Ligi jana
    Spacial Juan: Juan Mata celebrates helping his Chelsea boss extend his unbeaten record over Wenger
    Spacial Juan: Juan Mata akishangilia kumuwezesha kocha Chelsea kuendeleza ubabe wake kwa Wenger

    Once again: Didier Drogba heads past Phillippe Senderos in the 2007 League Cup final in another Mourinho win
    Mara nyingine tena: Didier Drogba akipiga kichwa pembeni ya Phillippe Senderos katika Fainali ya Kombe la Ligi mwakia 2007 katika mechi nyingine Mourinho anamfunga Wenger

    MOURINHO v WENGER


    Des 12 2004Arsenal 2 Chelsea 2Ligi Kuu
    Apr 20 2005Chelsea 0 Arsenal 0Ligi Kuu
    Ago 7 2005Chelsea 2 Arsenal 1 Ngao ya Jamii
    Ago 21 2005Chelsea 1 Arsenal 0Ligi Kuu
    Des 18 2005Arsenal 0 Chelsea 2Ligi Kuu
    Des 12 2006Chelsea 1 Arsenal 1Ligi Kuu
    Feb 25 2007Chelsea 2 Arsenal 1Fainali Kombe la Ligi
    Mei 6 2007Arsenal 1 Chelsea 1Ligi Kuu
    Okt 29 2013Arsenal 0 Chelsea 2Kombe la Ligi
    Katika mechi hiyo ya Kombe la Ligi, ambayo Arsenal ilibadilisha wachezaji nane wa kikosi cha kwanza na Chelsea 10 na bado Wenger alichapwa.
    Pat down: But Mourinho has fared poorly against Pep Guardiola over the years
    Ametulia chini: Lakini Mourinho naye ni kibonde wa Pep Guardiola

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER NI KIBONDE WA MILELE WA JOSE MOURINHO, HAKUNA UBISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top