• HABARI MPYA

    Wednesday, October 23, 2013

    ROBINHO NA NEYMAR 'WAFANYA YAO' SAN SIRO BARCELONA NA AC MILAN ZIKITOKA SARE YA 1-1 JANA

    WASHAMBULIAJI Neymar na Robinho walionekana kutaka sana kubadilishana jezi katika mechi baina ya timu zao, AC Milan na Barcelona Ligi ya Mabingwa jana usiku... na wakafanya hivyo wakati wa mapumziko!
    Licha ya kuchezea wote timu ya taifa ya Brazil, Robinho anabakia kuwa shujaa mkubwa wa Neymar na wawili hao walibadilishana jezi wakati refa anamaliza kipindi cha kwanza.
    Neymar alitoa heshima zake kwa winga wa Milan, anayemzidi miaka nane, kabla ya mchezo wa jana, lakini akamuonyesha kazi uwanjani.

    Mapema: Winga wa AC Milan, Robinho na mshambuliaji wa Barcelona, Neymar walibadilishana jezi wakati wa mapumziko jana

    Neymar aliposti picha yake akiwa mdogo pamoja na nyota huyo wa zamani wa Man City katika Instagram akisema: "Leo ni siku maalum kwangu...kwa kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya mkali wangu, ambaye nimekuwa nikimfuatilia wakati wote tangu nikiwa mdogo na ni heshima kucheza dhidi yake. Bahati nzuri wakati wote, lakini leo ni Barca hahahah, nakupenda,". 
    Wachezaji wote walianzia soka yao klabu ya Santos ya Brazil kabla ya kuhamia Ulaya kwa uhamisho wa fedha nyingi.
    Robinho alihamia Real Madrid mwaka 2005, akisajiliwa na vigogo hao wa Hispania kwa dau la Pauni Milioni 20 wakati Neymar alitua Barcelona mapema msimu huu kwa pauni Miloni 50.
    Through the years: Neymar posted a picture of himself with his hero Robinho on Instagram on Tuesday
    Miaka hiyo: Neymar ameposti picha yake akiwa na shujaa wake Robinho kwenye Instagram jana
    Pals: Robinho speaks with Neymar at the final whistle after Milan's 1-1 draw with Barcelona at the San Siro
    Pozi: Robinho akizungumza na Neymar baada ya mechi ya AC Milan na Barcelona Uwanja wa San Siro

    Wakati huo huo, mechi hiyo ya Kundi H iliisha kwa sare ya 1-1. Bahati mbaya kwa Neymar, alimshuhudia Robinho akiwafungia bao la kuongoza The Rossoneri dakika ya 10, baada ya mabaki wa Barca kujichanganya.
    Javier Mascherano alichanganyana na beki mwenzake Gerard Pique na Robinho akaunasa mpira kabla ya kugongeana pasi na Mbrazil mwenzake Kaka, kisha akafunga.
    Pamoja na hayo, bao la Milan halikudumu sana baada ya Lionel Messi kusawazisha dakika 13 baadaye.
    Ahead: Robinho takes full advantage of a mix-up in the Barcelona defence to put Milan 1-0 up
    Bao la kuongoza: Robinho alitumia mwanya wa mabeki wa Barcelona kujichanganya kuifungia Milan bao la kuongoza
    Robinho
    Goalscorer: Robinho celebrates putting the Rossoneri ahead during Milan's Group H match against Barcelona
    Mfungaji wa bao: Robinho akishangilia baada ya kuifungia The Rossoneri jana
    All level: Lionel Messi slides the ball past Marco Amelia in the Milan net to equalise for Barcelona
    La kusawazisha: Lionel Messi akimfunga kipa Marco Amelia kuisawazishia Barcelona
    Good finish: Messi is congratulated on his goal by Brazilian team-mates Dani Alves and Neymar
    Umalizijia mzuri: Messi akipongezwa na wenzake, Wabrazil Dani Alves na Neymar baada ya kufunga
    Halted: Ignazio Abate slide tackles Barcelona's Neymar and stops the Brazilian frontman in his tracks
    Ignazio Abate akiteleza kuondosha mpira miguuni mwa Neymar 
    Getting in the way: Milan players, including Mario Balotelli and Sulley Muntari, jump to stop Messi's free-kick
    Wacheaji wa Milan akiwemo Mario Balotelli na Sulley Muntari wakiruka kuzuia mpira wa adhabu wa Messi
    Late: Tough tackler Nigel De Jong powerfully challenges Andres Iniesta after the Spaniard had played the ball
    Nigel De Jong akipambana na Andres Iniesta 
    Battle: Robinho attempts to get past Barcelona full back Alves but has little success
     Robinho akipambana na Alves kugombea mpira
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROBINHO NA NEYMAR 'WAFANYA YAO' SAN SIRO BARCELONA NA AC MILAN ZIKITOKA SARE YA 1-1 JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top