• HABARI MPYA

    Wednesday, October 23, 2013

    HAMISI KIIZA 'DIEGO WA JANGWANI' BADO BAO MOJA TU KUMKAMATA TAMBWE SIMBA SC

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    HAMISI Friday Kiiza ‘Diego’ wa Yanga SC leo hii amefikisha mabao saba katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Rhino Rangers Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hii inakuwa mechi ya pili mfululizo Mganda huyo anafunga mabao mawili kila mechi, baada ya Jumapili pia kufunga mara mbili katika sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi, Simba SC Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hamisi Kiiza sasa ana mabao saba, moja tu nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba SC anayeongoza

    Kiiza sasa anazidiwa kwa bao moja tu mchezaji anayeongoza mbio hizo, Mrundi, Amisi Tambwe wa Simba SC, ambaye mechi tatu sasa hajafunga bao.  
    Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes analingana na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar ambaye pia ana mabao saba.
    Wanaofuatia ni Elias Maguri wa Ruvu Shooting mwenye mabao sita, Themi Felix wa Kagera Sugar mwenye mabao matano sawa na Tumba Swedi wa Ashanti, wakati Didier Kavumbangu wa Yanga SC ana ambao manne sawa na Kipre Tchetche Azam FC ambaye ndiye anashikilia tuzo ya ufungaji bora wa ligi hiyo.

    WANAOONGOZA KWA MABAO LIGI KUU:
    JINA                  TIMU MABAO
    Amisi Tambwe Simba SC 8
    Hamisi Kiiza Yanga SC 7
    Juma Luizio Mtibwa 7
    Elias Maguri Ruvu Shoot 6
    Themi Felix Kagera 5
    Tumba Swedi Ashanti 5
    D. Kavumbangu Yanga SC 4
    Kipre Tchetche Azam FC 4
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAMISI KIIZA 'DIEGO WA JANGWANI' BADO BAO MOJA TU KUMKAMATA TAMBWE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top