IMEWEKWA JUNI 5, 2013 SAA 11:35 ALFAJIRI
BEKI chipukizi wa Uganda, Samuel Ssenkoom (20) alitua Dar es Salaam juzi usiku tayari kujiunga na klabu ya Simba SC, baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili.
Ikumbukwe, Simba SC imekuwa ikihaha kuimarisha safu yake ya ulinzi tangu impoteze Kevin Yondan aliyenyakuliwa na watani, Yanga SC.
Mwanzoni mwa msimu uliopita, Simba SC ilimsajili Lino Masombo kutoka DRC, ikamtema, baadaye ikamsajili Mbuyu Twite kutoka Rwanda, lakini Yanga pia wakaingilia na kumbadili mawazo akageuza njia kwenda Jangwani alipo sasa.
Ikamsajili Paschal Ochieng kutoka Kenya, lakini haikuridhika naye ikamtema. Ikamsajili Komabil Keita naye pia haikuridhika naye ikamtema na katika mechi za mwishoni za msimu ikalazimika kuwapanga pamoja katika beki ya kati, Shomary Kapombe na Mudde, ambao kidogo walipunguza matatizo.
Baada ya kutua kwa Ssenkoom, sasa kocha mpya wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ atakuwa na jukumu la kumtafutia mtu sahihi wa kucheza naye pale katikati, kama atakuwa Kapombe ama Mudde au yeyote, ili mradi kutengeneza ukuta imara.
Hata hivyo, wakati mtazamo halisi ukipaswa kuwa huo kuhusu suluhisho la tatizo la beki ya kati ya Simba SC, katika siku ya kwanza tu jana akiwa mazoezini Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam, tayari maneno yameanza, tena ya kukatisha tamaa juu ya mchezaji huyo.
Na mbaya zaidi, wanaosema ni watu ambao unaweza ukawaita muhimu katika timu, watu ambao wanasikilizwa na wanaweza kusababisha lolote kwa mchezaji huyo. Wengine wanasema mzuri, lakini hana nyama. Wengine mzuri, lakini ni mfupi.
Kumbukumbu zinaonyesha beki ya kati ya Simba SC haijawahi kuitwa nzuri hata wakati Yondan yupo katika timu hiyo. ‘Wataalamu’ walikuwa wanasema, watu waliokuwa wanatumika kucheza beki ya kati wakati huo, walikuwa wa aina moja, yaani Juma Nyosso na Yondan na kwamba timu ilihitaji mtu mwingine wa kuwatenganisha ili kutengenza uwiano mzuri.
Ajabu hata Kapombe alipoletewa ‘jitu refu lenye miraba minne’, Lino Masombo bado tu watu hawakukosa kukosoa hadi Mkongo huyo akarudishwa kwao. Mimi bado nabaki kuwa miongoni mwa watu wanaoamini Lino alikuwa beki mzuri na Simba SC ilipoteza mtu wa maana katika safu yake ya ulinzi.
Simba SC wanapaswa kutambua kwamba, wametoka katika msimu mgumu na wanahitaji kujipanga upya taratibu, wawe na staha, uvumilivu na subira- vinginevyo msimu ujao hali itajirudia na kuzalisha migogoro zaidi klabuni, hivyo jahazi kuzidi kuzama.
Simba SC wameajiri kocha, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ au Chifu Mputa, tena mzuri na mzoefu kwa kuanzia kuucheza mpira na hata kuufundisha. Wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anashika mtutu jeshini kuipigania nchi yake dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada (sasa marehemu), King Kibadeni alikuwa mchezaji nyota Simba SC miaka ya 1970.
Alikuwa mshambuliaji bora na aliyekutana na mabeki bora barani Afrika na akaweza kufunga pamoja na mwili wake mdogo. Mimi naamini, kwa uzoefu wake pekee, Kibadeni anajua yupi ni beki bora. Kwa ujumla anajua yupi ni mchezaji mzuri. Simba SC wakimuachia King Kibadeni mustakabali wa timu, ataweza kuwavusha katika kipindi kigumu.
Wakati Kibadeni anaifikisha Simba SC fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, akiwa kocha, sentahafu wake alikuwa George Masatu, hakuwa mrefu na mwenye nyama. Sikatai, katika mpira wa leo, mabeki wa kati wanapaswa kuwa walioshiba, lakini bado mfumo mzuri wa uchezaji kulingana na aina ya wachezaji, unaweza kuziba mapungufu ya timu.
Miaka hii yote ambayo Barcelona ya Hispania imekuwa ikitawala soka ya Ulaya na duniani kwa ujumla, imekuwa ikielezewa beki yake ni butu, lakini imewezaje kutwaa mataji ya Ulaya, Dunia na Hispania? Mfumo mzuri wa uchezaji, kitimu ulioficha mapungufu binafsi ya watu katika timu ndio jibu.
Kutengeneza timu hadi ikawa madhubuti si jambo rahisi na si la muda mfupi, unahitajika muda na Simba SC lazima watambue hilo na kuweka subira kidogo, vinginevyo watarudi kule kule. Keita, Ochieng na Lino wote walikuwa wana miili mikubwa ambayo Ssenkoom hana, lakini wako wapi leo?
Sina utaalamu kiasi cha kuwashauri Simba SC wafanya nini juu ya kile ambacho wanaamini ni tatizo la kiufundi katika timu yao, zaidi ya kuwaambia, kazi ya kuijenga timu wamuachie kocha.
Nilivutiwa sana na maneno ya kocha Mreno aliyerejeshwa Chelsea, Jose Mourinho jana; “Tunatakiwa kuimarisha timu, na ninaposema naimarisha timu, watu tayari wanafikiria mamilioni mangapi Chelsea watatumia (kusajili).
“Lakini ninaposema naimarisha timu, nasema kuimarisha kwa kazi. Kazi yangu lazima iimarishe wachezaji na kuimarisha timu. Ikiwa sitafanya hivyo binafsi sitakuwa na furaha,”.
Hata Kibadeni anaweza kuiimarisha Simba SC bila uongozi kubomoa benki na kusajili wachezaji wa gharama. Kitu kimoja, Kibadeni ni mzuri sana katika kuibua vipaji na ndiye aliyewaibua wachezaji wengi ambao wanaelekea ukingoni hivi sasa akina Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan, Amir Maftah, Nurdin Bakari na wengineo, tena wakati huo hatuna haya mashindano ya vijana ya Copa Coca Cola wala Airtel Rising Star.
Kuendelea kumuona kila beki anayesajiliwa hafai ni kuzidi kuivuruga timu hiyo, maana beki ya Simba SC haikuwahi kusifiwa hata wakati ina Kevin Yondan. Alamsiki.

.png)