![]() |
| Adeyoum katikati akimshuhudia baba yake akitilia dole gumba kwenye fomu zake za usajili Simba SC. Kushoto ni Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Kinesi' |
BEKI aliyesali kuomba dua asajiliwe Simba SC, Adeyoum Saleh Ahmed dua yake imezaa matunda baada ya jioni ya leo kusainishwa Mkataba wa miaka mitatu kuchezea Wekundu hao wa Msimbazi.
Beki huyo wa Miembeni ya Zanzibar alitua kwenye majaribio Simba SC wiki iliyopita na kuanza kwa dua kocha Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ amkubali.
![]() |
| Adeyoum akiomba dua wakati wa majaribio |
![]() |
| Dua imepokewa...amesajiliwa Simba SC |
Baada ya wiki moja ya majaribio, hatimaye Adeyoum anayechezea pia timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes amefaulu na sasa anaelekea Msimbazi kuanza maisha mapya.
Adeyoum aliyezaliwa Septemba mwaka 1995 Zanzibar, kwa kuwa hajatimiza miaka 18, alisainiwa na baba yake mzazi leo Dar es Salaam Mkataba huo.







.png)