• HABARI MPYA

    Friday, April 19, 2013

    LIGI YA MABINGWA TANZANIA KUANZA MEI 12

    Tutashudhudia burudani kama hii Ligi ya Mabingwa bongo?

    Na Boniface Wambura
    LIGI ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
    Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
    Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata.
    Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA TANZANIA KUANZA MEI 12 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top