• HABARI MPYA

  Monday, April 01, 2013

  KITUKO CHA PASAKA CHA BALOTELLI, ALALA KWENYE SEHEMU YA MIZIGO NDANI YA TRENI NA FARAO


  MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alikuwa maarufu kwa vituko vyake na tabia za ajabu wakati akiwa Manchester City na anaonekana hajabadilika sana hata baada ya kurejea Italia.
  Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Ghana, alikutwa amelala kwenye eneo la juu la kuwekea mizigo ndani ya pamoja na wachezaji wenzake M'Baye Niang na Stephan El Shaarawy.
  El Shaarawy mwenye umri wa miaka 20, ambaye jina lake la utani ni 'Farao', amebandika picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwa amelala eneo la kuwekea mizigo na wachezaji wenzake hao wa Milan.
  Unorthodox: Mario Balotelli (left), M'Baye Niang (right) and Stephan El Shaarawy sleep in a luggage rack
  Machizi: Mario Balotelli (kushoto), M'Baye Niang (kulia) na Stephan El Shaarawy wakiwa wamelala eneo la kuwekea mizigo wakati siti zipo wazi.

  MILAN YAILAZA CHIEVO

  Soma taarifa ya AC Milan kuichapa bao 1-0 Chievo juzi Jumamosi HAPA
  Balotelli alijiunga na Milan  January baada ya misimu miwili na nusu ya kufanya kazi Manchester na ameendelea kuwa maarufu tangu arudi nyumbani.
  Mshambuliaji huyo alifunga mabao mawili dhidi ya Udinese na amefunga mabao matano katika mechi za Serie A tangu wakati huo.
  Pia aliifungia mabao yote Italia wiki iliyopita ikishinda 2-0 katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Malta kabla hajaisaidia Milan kushinda 1-0 mbele ya Chievo Jumamosi na kuongeza matumaini ya timu yake kufuzu Ligi ya Mabingwa.
  Star: Balotelli helped Milan beat Chievo 1-0 in a Serie A encounter on Saturday
  Nyota: Balotelli ameisaidia Milan kuifunga Chievo 1-0 katika mechi ya Serie A Jumamosi
  Finding the target: The forward has been prolific since returning to his homeland
  Anapiga mabao tu: Mshambuliaji huyo amekuwa mwiba tangu arejee nyumbani
  Representing the nation: Balotelli scored both goals in Italy's 2-0 win against Malta last week
  Anawakilisha taifa: Balotelli alifunga mabao yote wakati Italia ikishinda 2-0 dhidi ya Malta wiki iliyopiya
  Representing the nation: Balotelli scored both goals in Italy's 2-0 win against Malta last week
  Balotelli katika mechi ambayo Italia iliifunga 2-0 Malta
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KITUKO CHA PASAKA CHA BALOTELLI, ALALA KWENYE SEHEMU YA MIZIGO NDANI YA TRENI NA FARAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top