• HABARI MPYA

    Saturday, March 06, 2021

    SIMBA SC YABISHA HODI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE NA EL-MERREIKH LEO SUDAN

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamebisha hodi Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, El-Merreikh Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza Kundi A, ikifuatiwa na AS Vita yenye pointi tatu sawa na Al Ahly ambazo zinamenyana usiku wa leo mjini Cairo, wakati Merreikh yenye pointi moja inashika mkia.
    Mechi mbili za awali, Simba SC ilishinda 1-0 zote nyumbani na ugenini ikiwaadhibu AS Vita Jijini Kinshasa kwa bao la penalti mshambuliaji Mkongo Chris Kope Mutshimba Mugalu na Al Ahly Jijini Dar es Salaam kwa bao la kiungo wa  kimataifa wa Msumbini, Luis Miquissone.
    Sasa Simba SC inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa itarejea Dar es Salaam kwa mechi mbili mfululizo za nyumbani dhidi ya Al Merreikh Machi 16 na Vita Club Aprili 2, kabla ya kwenda kucheza mechi ya mwisho na Al Ahly Aprili 9 Jijini Cairo.
    Kikosi cha El Merreikh kilikuwa; Monged Abuzaid, Bakhit Khamis, Hamza Dawood/ Ramadan Agab dk12, Abdelrahman Hassan, Ahmad Adam Mohammad, Ahmed Mohamed, Tony Edjomariegwe, Tajeldin Elnour, Saifeldin Bakhit, Wagdi Allan na Darren Mattocks/ Al-Gozoli Nooh dk69.
    Simba SC; Beno Kakolanya, Pascal Wawa, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Larry Bwalya/ Hassan Dilunga dk61, Clatous Chama/ Francis Kahata dk77, Luis Miquissone, Muzamil Yassin/ Erasto Nyoni dk61, Thadeo Lwanga, Kope Mugalu/Meddie Kagere dk89.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YABISHA HODI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE NA EL-MERREIKH LEO SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top