• HABARI MPYA

    Saturday, December 19, 2020

    SERIKALI YAMPONGEZA MISS TANZANIA NA KUMTAKIA HERI KATIKA MASHINDANO YA DUNIA

    Na Shamimu Nyaki – WHUSM, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashugwa amempongeza Miss Tanzania 2020, Rose Manfere kwa kutwaa taji hilo na kumshauri kutumia urembo wake kuitangaza nchi vizuri.
    Waziri Bashungwa ametoa pongezi hizo leo Desemba 19, 2020 Jijini Dar es Salaam alipokutana na Mrembo huyo ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kumpa ushirikiano katika kutekeleza wajibu wake kwa Taifa kwa kuwa kwa sasa amebeba dhamana ya kutangaza nchi kwenye tasnia hiyo.
    “Serikali tutakuunga mkono katika jukumu hili ulilopata la kupeperusha Bendera ya nchi katika tasnia ya urembo kwa mwaka mmoja, nasisitiza tumia firsa hii kutangaza utamaduni wetu, mila na desturi za taifa letu na zaidi utalii unaopatikana hapa nchini”alisema Mhe.Bashungwa.


    Waziri Innocenti Bashungwa akizungumza na Miss Tanzania, Rose Manfere (kulia) leo ofisi ndogo ya Waziri huyo Jijini Dar es Salaam

    Aidha Bashungwa amempongeza Mratibu wa Mashindano hayo, Basilla Mwanukuzi kwa kuendesha mashindano hayo kwa weledi ambayo yamefanikisha kupatikana kwa mwakilishi wa kutangaza nchi na katika mashindano ya Urembo ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2021.
    Naye Mratibu wa Mashindano hayo Bi. Basilla Mwanukuzi ameishukuru Serikali kwa kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha mashindano hayo ambapo ameahidi kuwa Mrembo huyo atafanya vizuri katika mashindano ya Dunia.
    “Watanzania naomba tutoe ushirikiano kwa Mrembo huyu katika kazi yake ya kuitangaza nchi yetu kupindia urembo, akifanikiwa nchi pia imefanikiwa hivyo tumuunge mkono” alisema Bi Basilla.
    Mashindano hayo yamefanyika yamefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Slaam.


    Waziri Innocenti Bashungwa, Naibu wake, Abdallah Ulega, Katibu Mkuu, Dk. Hassan Abbasi na Mratibu wa Miss Tanzania, Basilisa Mwanukuzi katika picha ya pamoja na Miss Tanzania, Rose Manfere leo Dar es Salaam
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAMPONGEZA MISS TANZANIA NA KUMTAKIA HERI KATIKA MASHINDANO YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top