TIMU ya soka ya Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA U17 baada ya sare ya 1-1 na Djibouti Uwanja wa Umuganda mjini Rubavu, Rwanda.
Serengeti Boys iliyoanza na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Rwanda kwa ushindi huo, inafikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili kwenye michuano hiyo ambayo bingwa wake atacheza fainali za AFCON U17 zitakazofanyika Julai mwakani nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment