• HABARI MPYA

  Thursday, July 19, 2018

  SINGIDA UNITED WAENDA MWANZA KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United leo inaondoka Singida kwenda Mwanza kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba kikosi kizima cha timu hiyo kinaondoka kwa basi lake leo kwenda Mwanza.
  Sanga amesema kwamba hiyo itakuwa fursa nzuri kwa kocha wao mpya, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuinoa timu hiyo kikamilifu kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo Mei.
  Sanga amesema Morocco hajapata fursa nzuri ya kuinoa vizuri timu hiyo kwa sababu alianza nayo ikiwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya na kutoka hapo akaingia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
   
  “Tunaomba mashabiki na wadau wa soka, waandishi wa habari kutupa ushirikiano wakati wote wa maandalizi ya kuelekea kuanza msimu mpya wa ligi 2018/2019,”amesema Sanga.
  Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kwamba wakiwa mjini Mwanza wanatarajia kutangaza kikosi chao kamili, wachezaji wote wapya waliosajiliwa na walioondoka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAENDA MWANZA KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top