• HABARI MPYA

  Thursday, July 19, 2018

  OXLADE-CHAMBERLAIN KUUKOSA MSIMU WOTE UJAO LIVERPOOL

  KIUNGO Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kuukosa msimu wote ujao kutokana na maumivu ya goti kwa mujibu wa taarifa iliyotoka jana.
  Kiungo huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 24, aliumia goti katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Roma mwezi Aprili.
  Yalikuwa ni maumivu makubwa katika goti lake la mguu wa kulia na mwanasoka huyo wa kimataifa wa England ambaye alikwishaanza kuwa tegemeo la kocha Jurgen Klopp akakosa mechi zilizofuata.

  Maumivu ya goti yatamuweka nje msimu mzima Alex Oxlade-Chamberlain  

  Pamoja na goti, Oxlade-Chamberlain pia aliumia na nyama za paja na kufanyiwa upasuaji siku nane baada ya tukio na Daktari mtaalamu, Dk Andy Williams ambaye alisema anaweza kurejea November.
  Lakini taarifa za sasa zinasema kwamba Oxlade-Chamberlain ameambiwa anatakiwa kuwa nje kwa miezi 12 kuanzia sasa, maana yake hatapatikana msimu mzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OXLADE-CHAMBERLAIN KUUKOSA MSIMU WOTE UJAO LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top