• HABARI MPYA

  Monday, July 16, 2018

  MPAPPE AIKATAA REAL MADRID ASEMA ANABAKI PSG AKOMAE ZAIDI

  MSHAMBULIAJI chipukizi, Kylian Mbappe amekataa kuondoka Paris Saint-Germain msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa dunia. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa miongoni mwa nyota waliong'ara kwenye fainali za Kombe la Dunia na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi, akiweka rekodi ya mchezaji wa pili mdogo kufunga bao kwenye fainali ya Kombe la Dunia, baada ya Pele mwaka 1958, kikosi cha Didier Deschamps' kikiifunga Croatia 4-2. 
  Kiwango cha Mbappe kimemfanya ahusishwe na Real Madrid, ambayo inatafuta Galactico mwingine, baada ya kumruhusu Cristiano Ronaldo kujiunga na Juventus kwa ada ya Pauni Milioni 100.

  Kylian Mbappe amekataa kuondoka Paris Saint-Germain msimu huu kuhamia Real Madrid  

  Pamoja na hayo baada ya fainali, Mbappe amesema kwamba hana mpango msimu huu. 
  "Nitabaki PSG, kuendelea nao,"Mbappe aliwaambia Waandishi wa Habari. "Nipo mwanzoni mwa maisha yangu ya soka,". 
  Real Madrid pia imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na Neymar kumsajili msimu huu katika jitihada za kumtafuta nyota wao mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MPAPPE AIKATAA REAL MADRID ASEMA ANABAKI PSG AKOMAE ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top