• HABARI MPYA

    Thursday, July 19, 2018

    MAN UNITED NDIYO KLABU TAJIRI ZAIDI YA SOKA DUNIANI

    Manchester United kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye orodha ya klabu tajiri za michezo duniani 


    ORODHA YA KLABU 10 TAJIRI DUNIANI 

    1. Dallas Cowboys Pauni Bilioni 3,67 (NFL)
    2. Man Utd Pauni Bilioni 3.16 (soka)
    3. Real Madrid Pauni Bilioni 3.14 (soka)
    4. Barcelona Pauni 3.11 (soka)
    5. New York Yankees Pauni Bilioni 3.07 (MLB)
    6. New England Patriots Bilioni 2.84 (NFL)
    7. New York Knicks Pauni Bilioni 2.76 (NBA)
    8. Los Angeles Lakers Pauni Bilioni 2.53 (NBA)
    8. New York Giants, Pauni Bilioni 2.53 (NFL)
    10. Golden State Pauni Bilioni 2.38 (NBA) 
     30. Man City Pauni Bilioni 1.89 (soka)
     39. Arsenal Pauni Bilioni 1.71 (soka)
    46. Chelsea Pauni Bilioni 1.58 (soka)
    KLABU ya Manchester United imekuwa timu ya pili tajiri duniani miongoni mwa klabu za michezo, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
    Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ina thamani ya Bilioni 3.16 kwa mujibu wa jarida hilo, ikizizidi Real Madrid, Bayern Munich na Manchester City.
    United ilishindwa kutwaa kutwaa taji lolote msimu uliopita ikimaliza Ligi Kuu inazidiwa kwa pointi 19 na jirani zao, Man City, lakini bado imekuwa bidhaa adimu sokoni. 
    Washindi hao wa taji la Europa League mwaka 2017 wapo mbele ya vigogo wote wa La Liga, Real Madrid na Barcelona kwenye orodha, ambao wanashika nafasi ya tatu na ya nne wakiwa wana thamani ya Pauni Bilioni 3.13 na Bilioni 3.11.
    Bayern Munich ndiyo klabu nyingine pekee nje ya klabu za Ligi Kuu ya England kuingia kwenye orodha hiyo ikiwa nafasi ya 12 kwa thamani yake ya Pauni Bilioni 2.35. 
    City ipo nafasi ya 30 (Pauni Bilioni 1.89), wakati Arsenal (Pauni Bilioni 1.71) ina thamani zaidi ya mahasimu wao wa London, Chelsea (Pauni Bilioni 1.58), wakiwa nafasi ya 39 na 46 kwenye orodha hiyo.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED NDIYO KLABU TAJIRI ZAIDI YA SOKA DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top