• HABARI MPYA

  Wednesday, July 18, 2018

  JOSHUA ATAKA KUZIPIGA 'KAVU KAVU' NA BONDIA MMAREKANI NEW YORK

  BONDIA bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Muingereza Anthony Joshua jana alikutana kwa mara ya kwanza na mpinzani wake ajaye, Alexander Povetkin mjini New York, lakini akaishia kutaka kupigana na mbabe mwingine wa uzito wa juu Marekani, Jarrell 'Big Baby' Miller baada ya wawili hao kubadilishana maneno.
  Anthony Joshua alikuwa anaonyesha mikanda yake ya dunia huku akitambulishwa na MC kwenye ukumbi wa mikutano, lakini nyuma yake Miller akawa anatoa maneno ya dhihaka. 
  Joshua alishindwa kuvumilia na kugeuka kuanza kujibizana, kiasi cha kutaka kukabidhi mikanda ili wazipige kavu kavu – lakini wakatenganishwa na shughuli ikaendelea.
  Anthony Joshua akijibizana na Jarrell 'Big Baby' Miller jana mjini New York, Marekani 
  Joshua anayeshikilia mikanda ya IBF, WBA na WBO anatarajiwa kukutana ulingoni na Alexander Povetkin Septemba 22, mwaka huu Uwanja wa Wembley mjini London.
  Mbabe wa Urusi, Povetkin alimbwaga bondia David Price katika pambano la utangulizi kabla ya Joshua kuzipiga na Joseph Parker Machi mwaka huu na kushinda kwa pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA ATAKA KUZIPIGA 'KAVU KAVU' NA BONDIA MMAREKANI NEW YORK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top