• HABARI MPYA

    Wednesday, July 18, 2018

    HII RATIBA YA UHAKIKA LIGI KUU, AU MAMBO YATAENDELEA KUWA PANGA PANGUA?

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi leo limetoa ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itaanza Agoati 22, mwaka huu.
    Katika ratiba hiyo, mahasimu wa wa jadi, Simba na Yanga watakutana Septemba 30, mwaka huu katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ligi Kuu msimu wa 2018-2019 inatarajiwa kuanza Agosti 22, ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya mabingwa watetezi, Simba SC dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC), Mtibwa Sugar ambao utafanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Agosti 18.
    Mechi za ufunguzi za Ligi Kuu zitachezwa Agosti 22 kati ya Ruvu Shooting na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Alliance na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Coastal Union na Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. 
    Mechi nyingine ni kati ya Singida United na Biashara United Uwanja wa Namfua, Singida, Kagera Sugar na Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba zote Saa 10:00 jioni na Simba SC na Tanzania Prisons Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
    Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu utakamilishwa Agosti 23 kwa mechi kati ya JKT Ruvu na KMC Saa 8:00 mchana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stand United na African Lyon Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Mtibwa Sugar na Yanga SC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Azam FC dhidi ya Mbeya City Saa 1:00 usiku.
    Mtendaji Mku wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema kwamba msimu huu Ligi itaanza Agosti 22, 2018 na kufikia tamati Mei 19, mwakani (2019) ikiwa na jumla ya mechi 380 kutoka 240 msimu uliopita baada ya ongezeko la timu nne kutoka 16 za msimu uliopita.
    Pamoja na Wambura kutoa ratiba hiyo leo ikionyesha Ligi itaanza Agosti 22 na kufikia tamati Mei 19, lakini huo ni mtihani mkubwa kwao, kwani miaka ya karibuni ratiba zimekuwa zikipanguliwa mara kwa mara.
    Msimu uliopita ndiyo Ligi Kuu ilikuwa haieleweki kabisa, ratiba ziliokuwa zikipanguliwa mara kwa mara hadi ikafikia kukawa hakuna uhakika kabisa wa mechi kufanyika hadi ithibitishwe na Bodi.
    Swali la kujiuliza baada ya ratiba kutoka leo, Bodi na TFF wamejifunza kutokana na makosa ya misimu iliyotangulia na sasa wamekuja na ratiba ambayo wataiheshimu haitapanguliwa ovyo?
    Bila shala hilo ni jambo la kusubiri na kuona.  

    RATIBA KAMILI YA LIGI KUU HII HAPA








    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HII RATIBA YA UHAKIKA LIGI KUU, AU MAMBO YATAENDELEA KUWA PANGA PANGUA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top