• HABARI MPYA

  Tuesday, July 17, 2018

  AZAM TV ITAENDELEA KUONYESHA LIGI KUU MSIMU UJAO NA AZAM FC ITASHIRIKI KAMA KAWAIDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Azam TV imesema kwamba itaendedelea kuuheshimu na kuutekeleza mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu ya Bara kulingana na mabukubaliano yao na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Mkurugenzi wa Azam TV, Yussuf Bakhresa amesema kwamba wataendelea kuonyesha mechi za Ligi Kuu chini ya udhamini wa kampuni yoyote kulingana na makubaliano yao na TFF.
  “Jukumu letu ni kuonyesha mechi za Ligi Kuu, hilo tutaendelea kulitekeleza kama ambavyo tumekuwa tukifanya miaka yote. Na zaidi ninachoweza kusema ni kwamba watazamaji wetu watarajie mambo mazuri zaidi,”amesema Bakhresa akizungumza kwa simu kutoka Dubai jioni hii.

  Yussuf Bakhresa amesema kwamba wataendelea kuonyesha mechi za Ligi Kuu chini ya udhamini wa kampuni yoyote  

  Bakhresa amesema kwamba wamekuwa wakipokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau juu ya mapungufu kadhaa katika uonyeshaji wa mechi za Ligi Kuu na nyingine nyingi na wakati wote wamekuwa wakiyafanyia kazi.
  “Hadi sasa tunaridhishwa na kiwango chetu, lakini tumekuwa tukipokea maoni juu ya mapungufu madogo madogo na tumekuwa tukiyafanyia kazi. Na tutaendelea kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha tunawafikishia watazamaji wetu matangazo bora kabisa,”.
  Katika hatua nyingine, Bakhresa pia amesema kwamba wamefurahishwa na mafanikio ya klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Bara kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo.
  Azam FC ilibeba taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,  – maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Julai 13, mwaka huu.
  Na Bakhresa amesema kwamba hayo ni matunda ya uwekezaji wao mzuri katika timu, lakini pia kushiriki Ligi Kuu nzuri yenye ushindani. “Azam FC itakuwa na maandalizi mazuri kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu, lengo ni kuhakikisha inafanya vizuri na kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo,”amesema Bakhresa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV ITAENDELEA KUONYESHA LIGI KUU MSIMU UJAO NA AZAM FC ITASHIRIKI KAMA KAWAIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top