• HABARI MPYA

  Tuesday, July 17, 2018

  AJAX YAMREJESHA DALEY BLIND KWA PAUNI MILIONI 18

  KIUNGO Daley Blind anakaribia kurejea Ajax baada ya jana usiku Manchester United kukubaliana na klabu huyo ya Uholanzi.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 28 aliondoka kwa vigogo hao wa Amsterdam miaka minne iliyopita kuhamia Old Trafford kwa dau la Pauni Milioni 14.
  Blind amecheza mechi 141 United katika kipindi hicho, lakini msimu uliopita alicheza mechi saba tu za Ligi Kuu kwenye kikosi cha kocha Jose Mourinho.

  Daley Blind anakaribia kurejea Ajax baada ya Manchester United kumuuza  

  Na kwa sababu hiyo sasa anarejea klabu yake iliyomuibua na Man United wamethibitisha kukubaliana na Ajax juu ya uhamisho huo utakaogharimu Pauni Milioni 14.1 ambazo zinaweza kuongezeka hadi Milioni 18.5.
  Blind atakuwa mchezaji wa kwanza mkubwa kuondoka United msimu huu, ingawa Nahodha Michael Carrick amestaafu na kujiunga na benchi la Ufundi la Mourinho.
  Wakati huo huo; United imesajili wachezaji wapya watatu ambao ni Diogo Dalot kutoka Porto, Fred kutoka Shakhtar Donetsk na kipa mkongwe, Lee Grant kutoka Stoke City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AJAX YAMREJESHA DALEY BLIND KWA PAUNI MILIONI 18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top