• HABARI MPYA

    Friday, May 01, 2015

    GLAVU ZAZUA ZOGO PAMBANO LA PACQUIAO MAYWEATHER...MTU PESA HATAKI KUWASILISHA ZAKE ZIKAGULIWE

    MGOGORO umeibuka kuhusu glavu zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya pambano la utajiri la kihistoria katika ngumi za kulipwa.
    Kiasi cha saa 48 kabla ya kupanda ulingoni kuzipiga na Floyd Mayweather, kocha wa Manny Pacquiao, Freddie Roach amemlalamiki 'Mtu Pesa' hajawasilisha glavu zake zikaguliwe na Kamisheni ya MIchezo Nevada.
    Mayweather hajawasilisha glavu zake na mgogoro kama huo ulitokea kabla ya pambano lake na Marcos Maidana miezi 12 iliyopita.
    Pacquiao will wear a pair of Reyes gloves on Saturday; they are considered a puncher's glove
    Pacquiao atavaa glavu za Reyes kesho katika pambano lake na Mayweather

    GRANT vs REYES 

    Glavu zinazotengenezwa na Grant zinawapa ulinzi zaidi wa mikono mabondia kuliko nyingine; Hizi ni glavu nzuri kwa mabondia ambao walikuwa wana majeruhi ya mkono, kama afanyavyo Mayweather.
    Glavu za Reyes, zinazotengenezwa Mexico, zinaongeza uzito wa ngumi ya bondia. Hizi pia inamaanisha hazina ulinzi wa kutosha wa mikoni. 
    Katika pambano hilo, Mayweather alilalamikia glavu za mpinzani wake na mgogoro huo haukutatuliwa hadi asubuhi ya siku ya pambano
    Na Alhamisi, Roach akasema: "Nimewauliza Kamisheni ya Nevada kukagua glavu za mabondia wote. Glavu zao zinatengenezwa na Grant na za kwetu (zinatengenezwa) na Reyes. Nataka kuhakikisha glavu zao ziko sahihi.
    "Sasa glavu hazijaonyeshwa na bado ninataka kujua watatumia za aina gani"
    Kocha wa Mayweather, Floyd Snr, amepuuza malalamiko hayo akisema; "Glavu si ishu, kwa sababu Manny ana glavu kama hizo,"amesema. "Woga, ni hivyo tu. "(Kambi ya Pacquiao) imeendelea kuzungumza namna Floyd alikuwa anaogopa kwa miaka mitano, lakini walikuwa waoga. Hatukuwa waoga.' 
    Mayweather will wear a pair of custom-made gloves from manufacturers Grant on Saturday
    Mayweather will wear a pair of custom-made gloves from manufacturers Grant on Saturday
    Mayweather atavaa glavu za Grant kesho katika pambano na Manny
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GLAVU ZAZUA ZOGO PAMBANO LA PACQUIAO MAYWEATHER...MTU PESA HATAKI KUWASILISHA ZAKE ZIKAGULIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top