• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    MPINZANI WA BLATTER AKUTANA FARAGHA NA MALINZI HOTELI YA ‘KISHUA’ DAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MPINZANI wa Sepp Blatter katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Prince Ali Bin Al Hussein (pichani kushoto) jana alikutana faragha na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi.
    Blatter ni Rais wa FIFA, wakati Al Hussein ni makamu wake.
    Wawili hao walikutana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsinki (Hyatt) mjini Dar es Salaam- wazi Prince Ali Bin Al Hussein ambaye pia ni Rais Chama cha Soka Jordan (JFA), amekuja kuomba kura ya Tanzania katika Uchaguzi wa FIFA baadaye mwaka huu. 
    Malinzi amesema kKatika mazungumzo yao, zaidi waligusia maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Soka Jordan (JFA), hasa katika maeneo ya maendeleo ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.
    Al Hussein ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana kurudi nyumbani kwake Jordan baada ya kumwaga sera zake kwa Malinzi. Tayari TFF imekwishatangaza nia ya kumuunga mkono Blatter.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MPINZANI WA BLATTER AKUTANA FARAGHA NA MALINZI HOTELI YA ‘KISHUA’ DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top