• HABARI MPYA

    Saturday, December 27, 2014

    RUVU SHOOTING YAISHUSHA SIMBA SC BAADA YA KUICHAPA 1-0 JKT RUVU CHAMAZI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la Hamisi Suleiman limeipa ushindi wa 1-0 Ruvu Shooting dhidi ya ndugu zao, JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Suleiman alifunga bao hilo dakika ya 35 na sasa Ruvu Shooting inatimiza pointi 10 baada ya kucheza mechi nane na kupanda hadi nafasi ya saba, ikiishusha Simba SC yenye pointi tisa.
    JKT Ruvu inayobaki na pointi zake 10 baada ya mchezo huo wa nane, inabaki nafasi ya sita.  Katika mechi zilizotangulia jioni ya leo, Coastal Union imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Ruvu Shooting wamewalaza 1-0 JKT Ruvu

    Matokeo hayo, yanaifanya Coastal itemize pointi 12 baada ya kucheza mechi nane, wakati Prisons nayo inatimiza pointi saba baada ya mechi nane pia.
    Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, kati ya vinara Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu, Morogoro umevunjika dakika ya sita kutokana na mvua kubwa kunyesha. 
    TFF imeamua sasa mchezo huo utamaliziwa kesho. 
    Hadi Ligi Kuu inasimama baada ya raundi ya saba, Mtibwa Sugar walikuwa kileleni kwa pointi zao 15, wakifuatiwa na Azam FC na Yanga SC zilizofungana kwa pointi 13 kila moja na hata wastani wa mabao ukiwa sawa.
    Yanga SC na Azam zitamenyana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAISHUSHA SIMBA SC BAADA YA KUICHAPA 1-0 JKT RUVU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top