• HABARI MPYA

    Tuesday, December 23, 2014

    AFC LEOPARDS, GOR MAHIA ZAPIGANIA SAJILI YA MGANDA AUCHO

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    AFC Leopards na Gor Mahia za Kenya zimo mbioni kunasa huduma za kiungo wa timu ya taifa la Uganda na Tusker FC Khalid Aucho.
    Kwa mujibu wa wakala wake Fred Kajoba, Gor Mahia tayari imetuma ombi lake kunasa huduma za Aucho ambaye mkataba wake na Tusker umekamilika. Leopards pia walikuwa wamewasiliana na mchezaji huyo hapo awali.
    “Gor Mahia walinieleza wamtaka Aucho aijaze nafasi yake Geoffrey ‘Baba’ Kizito lakini Leopards pia wamtaka na kiungo mwenyewe afaa kwenda majaribio Qatar na vile vile Turkey muda wowote ujao,” Kajoba ambaye ni kocha wa magolikipa kwenye kikosi cha Cranes aliliambia BIN ZUBEIRY.
    Khalid Aucho anagombewa na Gor Mahia na AFC Leopards

    “Itabidi yeye, Aucho afanye uamuzi wa mapema manake kulingana na yeye Gor Mahia watamwongeza hela na upo uwezakano akapata namba kirahisi hivo atajiamulia mapema mwakani ila kwangu ningetamani sana asalie Tusker FC.”
    Kando na Aucho, Leopards pia imefanya mazungumzo na beki wa Tusker FC na mganda Martin Kiiza. Ingwe inasemekana ishamsajili golikipa wa Tusker FC Boniface Oluoch.
    Hayo yakijiri, straika chipukizi la Gor Mahia Timothy Otieno ataongoza mkataba wake na klabu hiyo baada ya wawili hao kuafikia maelewano.
    Otieno alijiunga na Gor Mahia kutoka klabu ya ligi ya daraja la pili FC Talanta mwezi Juni 2014 kwa mkopo wa miezi misita. Akiwa Gor Mahia, Otieno alicheza mechi 12 na kufunga bao moja tu dhidi ya Western Stima.
    “Tushazungumza na mwenyekiti (Ambrose Rachier) na tukaelewana kuongeza mkataba wangu,” mchezaji huyo wa timu ya taifa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka ishirini alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFC LEOPARDS, GOR MAHIA ZAPIGANIA SAJILI YA MGANDA AUCHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top