• HABARI MPYA

    Wednesday, December 24, 2014

    IVORY COAST WAGOMEA BAJETI YA SERIKALI KWA AJILI YA AFCON, WASEMA NI NDOGO

    Na Mwandishi Wetu, ABIDJAN
    SHIRIKISHO la Soka Ivory Coast (FIF) limegomea bajeti waliyopewa na Serikali ya nchi hiyo kwa ajili ushiriki wa timu ya taifa, The Elephants kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu ni ndogo.
    Serikali imekubali kutoa dola za Kimarekani 575 805 kwa Tembo wa Ivory Coast kwenye Fainali za AFCON zitakazofanyika Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 hadi Februari 8.
    Pamoja na hayo, Makamu wa rais wa FIF, Sory Diabate amewaambia Waandishi wa Habari jana kwamba; “Hatuwezi kwenda CAN (Mataifa ya Afrika) na faranga (za Ivory Coast, CFA Francs) Milioni 310. Tumewasilisha bajeti yetu kwa ufafanuzi mzuri,”amesema.
    Nyota wa Ivory Coast, Yaya Toure

    Waziri wa Michezo wa nchi hiyo alikuwa tayari kutoa fungu kamili waliloombwa katika bajeti ya awali faranga bilioni 3.5, pamoja na hayo Ivory Coast ilikwenda michuano hiyo mwaka 2013 Afrika Kusini na jumla ya Faranga bilioni 3.9, huku Serikali ikichangia Bilioni 2.7 wakati Tembo walitolewa na Nigeria katika Robo Fainali.
    Kikois cha Herve Renard, kitaanza maandalizi yake kwa kuweka kambi Abu Dhabi, Falme za Kiarabu Januari 5, mwakani. Ivory Coast imepangwa Kund D pamoja na Mali, Cameroon na Guinea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST WAGOMEA BAJETI YA SERIKALI KWA AJILI YA AFCON, WASEMA NI NDOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top