• HABARI MPYA

    Thursday, December 25, 2014

    ENYEAMA AWANIA KUWEKA BONGE LA REKODI AFRIKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA na Nahodha wa Nigeria, Vincent Enyeama ameingia kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji watatu kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka 2014.
    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza orodha ya mwisho ya wachezaji watatu katika siku ya leo ya Krisimasi na wapinzani wa Enyeama ni nyota wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na Mwanasoka Bora wa sasa Afrika, Yaya Toure wa Ivory Coast.
    Lakini Enyeama anatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa kiungo wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure ambaye bado anapewa nafasi ya kuendelea kuwa Mwanasoka Bora Afrika.
    Vincent Enyeama anawania kuwa kipa wa kwanza kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika baada ya miaka 28

    WANAOWANIA TUZO ZA CAF 2014  

    Mwanasoka Bora wa Afrika
    Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund)
    Vincent Enyeama (Nigeria na Lille)
    Yaya Toure (Ivory Coast na Manchester City)
    Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika
    Akram Djahnit (Algeria na ES Setif)
    El Hedi Belamieri (Algeria na ES Setif)
    Firmin Mubele Ndombe (DRC na AS Vita)
    Mwanasoka Bora wa Kike
    Annette Ngo Ndom (Cameroon na Amazon Grimstad)
    Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
    Desire Oparanozie (Nigeria na Guingamp)
    Mwanasoka Bora Chipukizi wa Kike
    Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
    Fabrice Ondoa (Cameroon na Barcelona)
    Uchechi Sunday (Nigeria na River Angels)
    Kipaji kinachoinukia vizuri zaidi
    Clinton N’jie (Cameroon na Olympique Lyon)
    Vincent Aboubakar (Cameroon na Porto)
    Yacine Brahimi (Algeria na Porto)
    Kocha Bora wa Mwaka
    Florent Ibenge (DRC)
    Kheireddine Madoui (ES Setif)
    Vahid Halilhodzic (kocha wa zamani wa Algeria)
    Timu ya Taifa ya Mwaka
    Algeria, Libya na Nigeria
    Timu bora ya taifa ya wanawake ya Mwaka
    Cameroon, Nigeria na Nigeria U-20
    Klabu Bora ya Mwaka
    Al Ahly (Misri), AS Vita (DRC) na ES Setif (Algeria)
    Watatu hao wamepigiwa kura na makocha, ama Wakurugenzi wa Ufundi wa timu za taifa barani Afrika au wawakilishi wa vyama vya soka vya nchi husika, kwa mujibu wa CAF.Wachezaji wawili, Ahmed Musa na Nahoha wa Ghana, Asamoah Gyan wamekomea kwenya tano bora na Enyeama anakuwa kipa wa kwanza kuingia kwenye tatu bora ya kuwania tuzo hiyo baada ya zaidi ya miongo miwili.
    Kipa huyo wa LOSC Lille ya Ufaransa anaweza pia kuwa mlinda mlango wa kwanza kushinda tuzo hiyo baada ya miaka 28 tangu gwiji wa Morocco, Badou Zaki, alipowashinda mchezaji mwenzake, Aziz Bouderbala na gwiji wa Cameroon, Roger Milla katika tuzo za mwaka 1986 wakati bado zinaandaliwa na Wafaransa.
    Mshindi atatangazwa katika usiku wa hafla maalum ya tuzo za CAF mjini Lagos, Nigeria Januari 8, mwakani. Katika Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika walioingia tatu bora ni Akram Djahnit (Algeria na ES Setif)
    El Hedi Belamieri (Algeria na ES Setif) na  Firmin Mubele Ndombe (DRC na AS Vita).
    Mwanasoka Bora wa Kike wanachuana Annette Ngo Ndom (Cameroon na Amazon Grimstad)
    Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels) na  Desire Oparanozie (Nigeria na Guingamp).
    Mwanasoka Bora Chipukizi wa Kike wanachuana  Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels),  Fabrice Ondoa (Cameroon na Barcelona) na Uchechi Sunday (Nigeria na River Angels).
    Kipaji kinachinukia vizuri zaidi wanachuana Clinton N’jie (Cameroon na Olympique Lyon), Vincent Aboubakar (Cameroon na Porto) na  Yacine Brahimi (Algeria na Porto).
    Kocha Bora wa Mwaka wanachuana  Florent Ibenge (DRC), Kheireddine Madoui (ES Setif) na Vahid Halilhodzic (kocha wa zamani wa Algeria). 
    Timu ya Taifa ya Mwaka ziachuana Algeria, Libya na Nigeria, Timu ya taifa ya wanawake ya Mwaka zinachuana Cameroon, Nigeria na Nigeria U-20, Klabu Bora ya Mwaka zinachuana Al Ahly (Misri), AS Vita (DRC) na ES Setif (Algeria).
    Yaya Toure anawania kutetea tuzo yake Mwanasoka Bora wa Afrika
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENYEAMA AWANIA KUWEKA BONGE LA REKODI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top