• HABARI MPYA

    Monday, December 29, 2014

    PHIRI ATIMULIWA KAZI SIMBA SC, KOPUNOVIC AJA JUMATANO KURITHI MIKOBA YAKE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSERBIA Goran Kopunovic atawasili Jumatano Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam.
    BIN ZUBEIRY inafahamu Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva kesho atakutaka na kocha Mzambia, Patrick Phiri kumtaarifu juu ya kumfuta kazi baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu chini yake.
    Na Kopunovic anatarajiwa kusaidiwa na Mnyarwanda, Jean Marie Ntagawabila- maana yake Suleiman Matola naye aliyekuwa msaidizi wa Phiri ataondolewa.
    Goran Kopunovic anakuja Jumatano kurithi mikoba ya Patrick Phiri 
    Patrick Phiri (kushoto) akiwa na Msaidizi wake Suleiman Matola kesho atapewa taarifa za kufutwa kazi

    REKODI YA PHIRI SIMBA SC TANGU AGOSTI 2014: 

    Simba SC 2-1 Kilimani City (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-0 Mafunzo (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr)
    Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-0 Ndanda (Kirafiki Mtwara)
    Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Stand United (Ligi Kuu)
    Simba SC 0-0 Orlando Pirates (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    Simba SC 2-4 Bidvest Wits (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-2 Jomo Cosmos (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Simba SC 0-0 Express (Kirafiki, Taifa)
    Simba SC 2-4 Mtibwa Sugar (Kirafiki, Chamazi)
    Simba SC 2-0 Yanga SC (Nani Mtani Jembe)
    Simba SC 3-1 Mwaduni United (Kirafiki, Taifa)
    Simba SC 3-1 Taifa Jang’ombe (Kirafiki, Zanzibar)
    Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bara)
    Kopunovic alifanya kazi kwa mafanikio nchini Rwanda akiwa na klabu ya Polisi kwa miaka mitatu kabla ya kuhamia Vietnam ambako pia alifanya kazi kwa mafanikio.
    Kocha huyo kijana anafundisha soka maridadi ya kuburudisha, kushambulia na sifa yake kubwa ni wachezaji wake kuwa na nguvu na kasi kutokana na aina ya mazoezi anayowapa.
    Kwa Ntagawabila, huyo ni kocha mwenye heshima kubwa Rwanda ambaye wakati fulani aliifanya APR iwe tishio mno kiasi cha kufikia kuifunga Zamalek ya Misri mabao 4-1 mwaka 2004 katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikitoka kufungwa 3-2 katika mchezo wa kwanza Cairo.
    APR ilisonga mbele hatua ya 16 Bora, ambako ilikwenda kutolewa kwa mbinde na Africa Sports ya Ivory Coast kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
    Simba SC inafikia hatua ya kuachana na Phiri baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu chini yake tangu ameanza kazi Agosti mwaka huu akirithi mikoba ya Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
    Simba SC iliachana na Logarusic kwa sababu tu ya tabia zake za kifedhuli, ambazo ilijaribu sana kumkemea, lakini hakuwa tayari kubadilika na ikaamua kumrejesha Phiri kutokana na historia yake ya kufanya kazi kwa mafanikio awali katika klabu hiyo. 
    Hata hivyo, safari hii mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa baina ya Phiri na Simba SC na ndoa yao inafikia tamati, Kopunovic akiingia kazini.
    Phiri aliiongoza Simba SC kwa mara ya mwisho Desemba 26, ikifungwa 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Jean Marie Ntagwabila atakuwa Msaidizi wa Kopunovic Simba SC  

    Tangu amekuja Simba SC kwa mara ya tatu Agosti mwaka huu, Phiri ameiongoza Simba SC katika mechi 22 na kushinda nane, kati ya hizo moja tu ya Ligi Kuu 1-0 dhidi ya Ruvu Shooitng na moja ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga SC 2-0, wakati amefungwa tano na kutoka sare tisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PHIRI ATIMULIWA KAZI SIMBA SC, KOPUNOVIC AJA JUMATANO KURITHI MIKOBA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top