• HABARI MPYA

    Tuesday, December 30, 2014

    LIVERPOOL YAICHAPA SWANSEA 4-1 ENGLAND

    TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Swansea usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Beki Mspanyola, Alberto Moreno aliifungia timu ya Brendan Rodgers bao la kwanza dakika ya 33, kabla ya Adam Lallana kufunga mawili dakika za 51 na 60 na Jonjo Shelvey kujifunga dakika ya 68 kuipatia Liverpool bao la nne.
    Bao pekee la Swansea lilifungwa na Sigurdsson dakika ya 52 na sasa Liverpool inatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 19, ingawa inabaki nafasi ya nane.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Manquillo, Henderson, Lucas, Moreno, Lallana/Markovic dk77, Coutinho/Borini dk89 na Sterling/Balotelli dk82.
    Swansea; Fabianski, Richards/Rangel dk46, Fernandez, Williams, Taylor, Britton/Ki dk66, Shelvey, Dyer, Sigurdsson, Routledge na Bony/Gomis dk62.
    The England international wheels away in celebration of his first goal of the night at Anfield
    Adam Lallana akishangilia baada ya kuifungia Liverpool jana Uwanja wa Anfield

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2890410/Liverpool-4-1-Swansea-Adam-Lallana-bags-brace-Jonjo-Shelvey-puts-net-torrid-return-Anfield.html#ixzz3NLrkYlAx 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA SWANSEA 4-1 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top