• HABARI MPYA

    Thursday, November 07, 2013

    UKUTA WA CHUMA UMEREJEA ARSENAL...WENGER SASA ANAKULA KIPUPWE TU EMIRATES

    Mertescker akimdhibiti Lewandowski jana
    KUTAJA mabeki wanne wanaounda ukuta wa Arsenal ni rahisi: Sagna, Mertesacker, Koscielny na Gibbs.
    Imemchukua miaka mingi kocha Arsene Wenger kurudisha ukuta mashubuti aliokuwa nao wakati anaanza kazi Septemba 1996. Hatimaye ameweza.
    Iwe kwa bahati au uamuzi, ana mabeki wanne ambao vijana wadogo wanaocheza kwa uelewano na hawataki kuruhusu mabao.
    Arsenal's Per Mertesacker
    Arsenal's Laurent Koscielny
    Ukuta kweli: Mertesacker (juu kushoto), Koscielny (juu kulia), Gibbs (chini kushoto) na Sagna (chini kulia) sasa ni ukuta mpya tishio Arsenal
    Kieran Gibbs of Arsenal
    Bacary Sagna of Arsenal
    Hizo ni zama ambazo Dixon, Adams, Bould au Keown na Winterburn walikuwa wanaunda ukuta bora wa Arsenal uliofanya timu hiyo itambe katika Ligi Kuu ya England na kujizolea umaarufu Ulaya nzima.
    Usiku wa jana Uwanja wa Westfalenstadion, dhidi ya Borussia Dortmund iliyofungwa katika fainali ya msimu uliopita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ulikumbushia enzi za ukuta mgumu wa Asrenal. 
    Angalia rekodi yao msimu huu na rahisi kuelewa kwa nini wanaongoza kwa pointi tano zaidi kileleni mwa Ligi Kuu ya England na wanaongoza Kundi F katika Ligi ya Mabingwa.
    Wameruhusu mabao 12 katika mechi 16 kwenye mashindano yote tangu mwanzoni mwa msimu huu.
    Arsenal's Martin Keown
    TONY ADAMS
    Wakali wa kale: Keown (juu kushoto), Adams (juu kulia), Winterburn (chini kushoto) na Dixon (chini kulia) huu ulikuwa ukuta tishio wa Arsenal siku za mwanzo za Wenger katika timu hiyo
    NIGEL WINTERBURN
    LEE DIXON
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UKUTA WA CHUMA UMEREJEA ARSENAL...WENGER SASA ANAKULA KIPUPWE TU EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top