SAFARI ya Celtic kwenda kumenyana na Ajax kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa ilikuwa chungu baada ya mashabiki wao kushambuliwa na Polisi katikati ya Jiji la Amsterdam kabla ya mechi, ikifuatiwa na mashabiki 15 kukamatwa.
Polisi yaAmsterdam imesema kwamba mashabiki hao walikuwa wana chupa na fimbo wakipanga kushambulia kabla ya kuwahiwa na askari.
Polisi nane walijeruhiwa na mmoja kuumizwa vibaya katika mapambano yaliyotokea Dam Square, katikati ya Jiji.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mjini Amsterdam kabla ya mechi

Mashabiki wa Celtic walikuwa wana bonge la pati mjini Amsterdam kabla ya mechi na Ajax

Celtic ilifungwa 1-0 katika mechi hiyo na sasa wanakabiliwa na kibarua kizito kufuzu hatua ya mtoano.
Polisi wa Amsterdam walisema wanatarajia idadi ya mashabiki 15 waliokamatwa itaongezeka. Maelfu ya mashabiki wa Celtic walitua Uholanzi kwa ajili ya mchezo huo wa Kundi H Uwanja wa Amsterdam Arena.

Polisi wakiwa tayari kwa mapambano na mashabiki Dam Square

Shabiki huyu akisalimu amri mbele ya Polisi kwa kupiga magoti

Shabiki huyu wa Celtic akisongeshwa na Polisi wa kike

Mashabiki wakiangalia kutokea ndani ya baa wakati Polisi wanapita



.png)
0 comments:
Post a Comment