• HABARI MPYA

    Monday, November 11, 2013

    TATHMINI YA MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU BARA, YANGA BADO MOTO WA KUOTEA MBALI

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    YANGA SC iliongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya mechi za kwanza za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Ashanti United, zote za Dar es Salaam.
    JKT Ruvu ikapaaa kileleni baada ya mechi za pili na ikadumu hadi mzunguko wa tano ilipoipisha Simba SC. Angalau Simba SC ilidumu kwa muda mrefu huko hadi mzunguko wa 10, ilipozipisha Azam FC na Mbeya City.
    Simba SC ikajivuruga na kujikuta inapotea kabisa ndani ya tatu bora, ikizipisha Azam, Mbeya City na Yanga SC.
    Yanga ikarejea kileleni baada ya mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza, kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya JKT Oljoro, huku Azam na Mbeya City zikitoshana nguvu kwa sare ya 3-3.
    Pointi 28 zinaifanya Yanga iliyoanzia kileleni baada ya mechi za kwanza kumalizia kileleni pia, ikizizidi kwa pointi moja moja Azam na Mbeya City.  
    Vinara na watetezi; Yanga SC wamemaliza kileleni mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Bara

    YANGA SC;
    Ilianza Ligi vyema, lakini ikaingia kwenye wimbi la sare mfululizo, kabla ya kuzinduka na kufanya kweli, hatimaye kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni na wazi Yanga ipo katika nafasi ya kutetea ubingwa wake kutokana na ubora wa timu na wachezaji wake. Katika mechi 13, imeshinda nane, sare nne, imefungwa moja na Azam FC, imefunga mabao 31, imefungwa 11 na imemaliza na pointi 28 
                   P W D L GF GA GD Pts
    1 Yanga 13 8 4 1 31 11 20 28

    AZAM FC;
    Haikuwa na mwanzo mzuri sana, lakini baadaye ikasimama imara na kupanda kileleni kabla ya kuja kuenguliwa na Yanga SC siku ya mwisho ya mzunguko wa kwanza. Pamoja na hayo, Azam bado ni timu imara na inaweza kutimiza ndoto zake za kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Bara msimu huu, licha ya kumpoteza kocha wake, Muingereza, Stewart Hall aliyejiuzulu siku ya mwisho. Katika mechi 13, imeshinda saba, sare sita, haijafungwa hata moja, imefunga mabao 23, imefungwa 10 na imemaliza na pointi 27. 
                  P W D L GF GA GD Pts
    2 Azam 13 7 6 0 23 10 13 27

    MBEYA CITY;
    Imekuwa na mwanzo mzuri katika Ligi Kuu, ikipanda msimu huu na kufanikiwa kuwa moja ya timu zilizo katika mbio za taji. City ingeweza kumaliza mzunguko wa kwanza kileleni kama isingeruhusu kusawazishiwa bao na Azam FC na kutoa sare ya 3-3 katika mechi ya mwisho. Bado ina nafasi ya kuvunja rekodi ya Tukuyu Stars ya Mbeya pia, iliyopanda Ligi Kuu na moja kwa moja kuchukua taji mwaka 1986. Katika mechi 13, imeshinda saba, sare sita, haijafungwa, imefunga mabao 19, imefungwa 10 na imemaliza na pointi 27.  
                           P W D L GF GA GD Pts
    3 Mbeya City 13 7 6 0 19 10 9 27

    SIMBA SC;
    Ilitoa sare katika mechi ya kwanza, lakini ikashinda mfululizo mechi zilizofuata hadi kukaa kileleni kwa muda mrefu, kabla ya kuenguliwa mwishoni na Azam FC na Mbeya City. Ilionekana zaidi kuathiriwa na migogoro baina ya wachezaji na benchi la ufundi, lakini ikiwa timu inayoundwa na yosso wengi, Simba SC ilionyesha ni timu inayoweza kubeba taji. Katika mechi 13, imeshinda sita, sare sita na kufungwa moja na Azam FC, imefunga mabao 26, imefungwa mabao 13 na imemaliza na pointi 24.
                         P W D L GF GA GD Pts
    4 Simba SC 13 6 6 1 26 13 13 24

    KAGERA SUGAR:
    Ilianza vibaya mzunguko wa kwanza, lakini baadaye ikasimama imara na kuanza kufanya vizuri, hatimaye kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tano. Huwezi kuifikiria ubingwa hata nafasi ya pili, lakini pia huwezi kuitabira kumaliza nje ya timu tano za juu mwishoni mwa msimu. Katika mechi 13,  imeshinda tano, sare tano na kufungwa tatu, imefunga mabao 15, imefungwa 10 na imemaliza na pointi 20.
                              P W D L GF GA GD Pts
    5 Kagera Sugar 13 5 5 3 15 10 5 20

    MTIBWA SUGAR;
    Ilianza kwa sare ya nyumbani na Azam, baadaye ikawa inashinda, inafungwa na kutoa sare. Kwa ujumla Mtibwa ikawa timu isiyotabirika na haikuwa ajabu kumaliza katikati ya msimamo. Bado huwezi kuifikiria kurudia kile ilichokifanya mwaka 1999 na 2000, kutwaa ubingwa wa Bara mfululizo. Katika mechi 13, imeshinda tano, sare tano, imefungwa tatu, imefunga mabao 19, imefungwa 17 na imemaliza na pointi 20.   
                               P W D L GF GA GD Pts
    6 Mtibwa Sugar 13 5 5 3 19 17 2 20

    RUVU SHOOTING;
    Ilikuwa na mwanzo mzuri, lakini baadaye ikaanza kusuasua na haikuwa ajabu kumaliza katikati ya msimamo. Bado ni timu inayocheza soka nzuri na ina wachezaji wazuri, ila huwezi kuitabiria hata kumaliza ndani ya tatu bora kwa sababu inaonekana kucheza ligi ili isishuke tu. Katika mechi 13, imeshinda nne, sare tano na kufungwa nne, imefunga mabao 15 na imefungwa 15, imemaliza na pointi 17.
                                P W D L GF GA GD Pts
    7 Ruvu Shooting 13 4 5 4 15 15 0 17

    COASTAL UNION;
    Baada ya usajili wa kishindo na mwembwe nyingi, ikaanza na ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya JKT Oljoro na kujiona iko vizuri, kumbe ilifunga vibonde. Mabingwa hao wa 1988 wakaanza kusuasua hadi kumfukuza kocha wake, Hemed Morocco na kuwa chini ya makocha wa muda, Joseph Lazaro na Razack Yussuf ‘Careca’. Katika mechi 13, imeshinda tatu, sare saba na kufungwa tatu, imefunga mabao 10, imefungwa saba na imemaliza na pointi 16. 
                               P W D L GF GA GD Pts
    8 Coastal Union 13 3 7 3 10 7 3 16

    JKT RUVU; 
    Ilikuwa timu ya pili kuongoza Ligi Kuu mzunguko wa kwanza msimu huu baada ya Yanga SC na ilianza vizuri kweli. Hata hivyo, inazidi kuthibitika sasa kwamba, JKT ni timu ambayo inacheza Ligi ili isishuke tu na haina malengo ya zaidi. Lakini ina uwezo ikiamua japo kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu, ila kwa mwenendo wake huwezi kuifikiria hivyo. Katika mechi 13, imeshinda tano, haina sare zaidi ya kufungwa mechi nane, imefunga mabao 10, imefungwa 16 na imemaliza na pointi 15. 
                        P W D L GF GA GD Pts
    9 JKT Ruvu 13 5 0 8 10 16 -6 15

    RHINO RANGERS;
    Ilionyesha ni timu nyingine nzuri baada ya kucheza vyema na kutoa sare na vigogo Simba SC katika mechi ya kwanza, lakini baadaye ikaanza kufungwa hadi nyumbani- maana yake, Tabora bado hawajapata cha kujivunia katika Ligi Kuu. Inaweza kushuka daraja isipojipanga vizuri katika mzunguko wa lala salama. Katika mechi 13, timu hiyo iliyopanda msimu huu imeshinda mbili, sare tano na kufungwa sita, imefunga mabao tisa, imefungwa 16 na imemaliza na pointi 11. 
                                  P W D L GF GA GD Pts
    10 Rhino Rangers 13 2 5 6 9 16 -7 11

    JKT OLJORO;
    Bila shaka huu unaweza kuwa msimu mbaya zaidi kwa timu hiyo inayocheza Ligi Kuu kwa msimu wa tatu sasa na wazi inapoelekea ni kushuka Daraja. Oljoro inaweza kuwa inacheza msimu wa mwisho wa Ligi Kuu, kwani pamoja na kuwa katika nafasi mbaya, pia haileti matumaini. Katika mechi 13, imeshinda mbili, sare nne, imefungwa saba, imefunga mabao tisa, imefungwa 19 na imemaliza na pointi 10. 
                           P W D L GF GA GD Pts
    11 JKT Oljoro 13 2 4 7 9 19 -10 10

    ASHANTI UNITED;
    Ilianza vibaya katika msimu wake iliyorejea Ligi Kuu, lakini baadaye ikasimama imara na kuonyesha kwamba inaweza kupambana. Japokuwa ipo nafasi ya tatu kutoka mkiani, lakini kutokana na kuimarika kwake siku hadi siku, Ashanti inatia matumaini ya kubaki Ligi Kuu. Katika mechi 13, imeshinda mbili, sare nne na kufungwa saba, wakati imefunga mabao 12, imefungwa 24 na imemaliza a pointi 10 pia.
                                  P W D L GF GA GD Pts
    12 Ashanti United 13 2 4 7 12 24 -12 10

    PRISONS;
    Imekuwa na mwanzo mwingine mbaya katika msimu wa pili tangu irejee Ligi Kuu na bila shaka msimu huu inaweza kushuka baada ya kunusurika msimu uliopita. Kwa kweli Prisons haileti matumaini hususan baada ya kufungwa hadi na JKT Oljioro nyumbani. Katika mechi 13, imeshinda moja tu, sare sita na kufungwa sita, wakati imefunga mabao sita na kufungwa 16, imemaliza na pointi tisa.
                       P W D L GF GA GD Pts
    13 Prisons 13 1 6 6 6 16 -10 9

    MGAMBO JKT:
    Imekuwa na mwanzo mwingine mbaya katika msimu wake wa pili tangu ipande Ligi Kuu na kulingana na hali halisi, Mgambo inaweza kuwa inacheza msimu wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara. Ndiyo inashika mkia baada ya kuvuna pointi sita tu katika mechi 13, ikishinda moja, sare tatu na kufungwa tisa. Kichekesho zaidi, imefunga mabao matatu wakati imefungwa 23.  
                                P W D L GF GA GD Pts
    14 Mgambo JKT 13 1 3 9 3 23 -20 6

    REKODI ZA MZUNGUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU BARA:
    AGOSTI 24, 2013;
    Juma Luizio amefunga bao la kwanza la msimu, dakika ya nne Mtibwa Sugar ikitoa sare ya 1-1 na Azam Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.  
    AGOSTI 24, 2013;
    Laurian Mpalile amekuwa mchezaji wa kwanza kujifunga dakika ya 23, Prisons ikifungwa 3-0 na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
    AGOSTI 24, 2013;
    Aggrey Morris amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwa penalti, akiisawazishia Azam FC dakika ya 19 katika sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.    
    AGOSTI 24, 2013;
    Emmanuel Kichiba wa Ashanti United amekuwa mchezaji wa kwanza kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 12, timu yake ikifungwa 5-1 na Yanga  
    SEPTEMBA 18, 2013;
    Amisi Tambwe amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick, akifunga mabao manne katika ushindi wa 6-0 wa Simba SC dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    SEPTEMBA 18, 2013;
    Crispin Odula wa Coastal Union na Simon Msuva wa Yanga SC wanakuwa wachezaji wa kwanza kutolewa kwa pamoja kwa kadi nyekundu baada ya kugombana dakika ya 77, timu zao, zikitoka sare ya 1-1. 
    SEPTEMBA 18, 2013;
    Kipa Abbel Dhaira wa Simba SC ametimiza mechi tatu za kudaka bila kufungwa hata bao moja, (Simba 1-0 JKT Oljoro, Simba 2-0 Mtibwa Sugar na Simba 6-0 JKT Mgambo).  
    SEPTEMBA 22, 2013;
    John Bocco ‘Adebayor’ amefunga bao la mapema zaidi, sekunde ya 34, Azam ikishinda 3-2 dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
    OKTOBA 13, 2013
    Abdallah Juma anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu peke yake katika mechi moja, Mtibwa Sugar ikishinda 5-0 dhidi ya JKT Oljoro Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    OKTOBA 20, 2013
    Yanga SC walikwenda kupumzika wanaongoza mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC lakini kipindi cha pili walitepeta na kusawazishiwa mabao yote, hadi wakaomba mechi iishe, kwani kwa kasi ya Wekundu wa Msimbazi katika dakika za mwishoni, wangeweza kupata mabao zaidi.   
    OKTOBA 31, 2013
    Simba SC v Kagera Sugar; Mechi hiyo ilihitimishwa kwa milipuko ya mabomu ya machozi, Polisi wakituliza ghasia, baada ya mashabiki wa Simba SC kuanza kung’oa viti kurusha uwanjani, kufuatia Kagera Sugar kusawazisha bao dakika ya pili ya muda wa nyongeza, baada ya kutimu dakika 90 na kupata sare ya 1-1.
    NOVEMBA 1, 2013
    Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC anavunja rekodi ya kipa Mganda Abbel Dhaira wa Simba SC kudaka mechi tatu mfululizo bila kufungwa, baada ya kudaka Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya Rhino, 3-0 na Mgambo na 4-0 mbele ya JKT Ruvu. 
    NOVEMBA 7, 2013
    Mwagane Yeya wa Mbeya City anafunga hatrick ya tatu ndani ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, katika sare ya tatu na Azam FC Uwanja wa Azam Complex.
    NOVEMBA 7, 2013
    Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC anaweka rekodi mpya msimu huu, baada ya kudaka mechi nne mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa (Yanga 3-0 Rhino, 3-0 Mgambo, 4-0 JKT Ruvu na 3-0 JKT Oljoro). 
    10 Juu; Amisi Tambwe ndiye kinara wa mabao Bara mzunguko wa kwanza 

    WALIOFUNGA MABAO MZUNGUKO WA KWANZA:
    JINA TIMU MABAO
    Amisi Tambwe Simba SC 10
    Hamisi Kiiza Yanga SC 8
    Juma Luizio Mtibwa 8
    Elias Maguri Ruvu Shoot 8
    Kipre Tchetche Azam FC 8
    Themi Felix Kagera 7
    Mrisho Ngassa Yanga SC 6
    Jerry Tegete Yanga SC 5
    Tumba Swedi Ashanti 5
    D. Kavumbangu Yanga SC 5
    Mwagane Yeya Mbeya City 5
    Bakari Kondo JKT Ruvu 4
    Betram Mombeki Simba SC 4
    Jerry Santo Coastal U 4pen
    Khamis Mcha Azam FC 4
    Abdallah Juma Mtibwa 3
    Haruna Chanongo Simba SC 3
    Paul Nonga Mbeya City 3
    Jeremiah John Mbeya City 3
    Peter Michael Prisons 3
    Machaku Salum JKT Ruvu 3
    Jonas Mkude Simba SC 3(1pen)
    Amiri Hamad JKT Oljoro 3
    John Bocco Azam FC 3
    Joseph Kimwaga Azam FC 2
    Salum Kanoni Kagera Sugar 2penalti
    Crispin Odula Coastal U 2
    Gilbert Kaze Simba SC 2
    Richard Peter Mbeya City 2
    Saad Kipanga Rhino 2
    Imani Noel Rhino 2
    Haruna Moshi Coastal U 2
    Shaibu Nayopa JKT Oljoro 2
    Malimi Busungu JKT Mgambo 2
    Godfrey Wambura Kagera 2
    Shaaban Kisga Mtibwa Sugar 2
    Said Dilunga Ruvu Shoot 2
    Selemani Kibuta Kagera 2
    Daudi Jumanne Kagera 1
    Maregesi Mwangwa Kagera 1
    Salum Abubakar Azam FC 1
    Erasto Nyoni Azam FC 1
    Henry Joseph Simba SC 1
    Ramadhani Singano Simba SC 1
    Joseph Owino Simba SC 1
    Expedito Kiduko JKT Oljoro 1
    Paul Malipesa JKT Oljoro 1
    Nurdin Mohamed JKT Oljoro 1
    Fikiri Mohamed JKT Oljoro 1
    Simon Msuva Yanga SC 1
    Haruna Niyonzima Yanga SC 1
    Oscar Joshua Yanga SC 1
    Frank Domayo Yanga SC
    Nizar Khalfan Yanga SC 1
    Abdi Banda Coastal U 1
    Danny Lyanga Coastal U 1
    Shaaban Juma Ashanti 1
    Paul Maona Ashanti 1
    Anthony Matangalu Ashanti Utd 1
    Mwinyi Ally Ashanti Utd 1
    Mussa Nampaka Ashanti Utd 1
    Samir Ruhava Ashanti Utd 1(kujifunga)
    Aggrey Morris Azam FC 1pen 
    G. Mwaikimba Azam FC 1
    Farid Malik Azam FC 1
    Seif Abdallah Azam FC 1
    Humphrey Mieno Azam FC
    Fully Maganga Mgambo 1
    Emanuel Swita JKT Ruvu 1
    Hussein Bunu JKT Ruvu
    Amos Mgisa JKT Ruvu 1
    Laurian Mpalile Prisons 1(kujifunga)
    John Matei Prisons 1
    Samir Luhava Ashanti Utd 1(kujifunga)
    Jerome Lambele Ruvu Shoot 1
    Shaaban Suzan Ruvu Shoot 1
    Cosmass Lewis Ruvu Shoot 1
    Steven Mazanda Mbeya City
    Salum  Majid Rhino 1
    Hamisi Msafiri Rhino 1
    Kamana Salum Rhino 1
    Hussein Abdallah Rhino 1
    Peter Mapunda Mbeya City 1
    Masoud Ally Mtibwa 1
    Salum Mkopi Mtibwa 1
    Salim Mbonde Mtibwa 1

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TATHMINI YA MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU BARA, YANGA BADO MOTO WA KUOTEA MBALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top