KLABU ya Barcelona ilimudu kushinda 4-1 dhidi ya Real Betis licha ya Lionel Messi kuumia mapema.
Messi alipata matatizo wakati akikimbia na mpira dakika ya 18 - majeruhi ya tatu ya mguu wake msimu huu.
Neymar na Pedro walifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili kipindi cha kwanza na Cesc Fabregas akakamilisha ushindi mnono kwa mabao mawili ya kipindi cha pili, kabla ya Jorge Molina kuifungia kwa penalti Betis dakika za majeruhi.
Hakuna tatizo: Lakini Barca ilishinda

Wamefunga: Mabao ya Neymar, Pedro na mawili ya Cesc Fabregas waliipa timu hiyo ushindi mnono


Anatoka: Alitolewa dakika ya 21




.png)
0 comments:
Post a Comment