MASHABIKI wa Arsenal wakiambiwa wachague nyota mmoja wa klabu yao wa kukutana naye na kumalimia, bila shaka nyota wa Ujerumani, Mesut Ozil atakuwa matawi ya juu katika orodha ya watakaochaguliwa.
Lakini shabiki mmoja aliyekuwa amevaa jezi ya Gunners yenye jina la mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mgongoni - inaonekana alikosa kitu, japokuwa alikuwa eneo hilo hilo.
Ozil alikuwa akishangilia ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya Liverpool akiwa mpenzi wake, Mandy Capristo. Kiungo huyo Mjerumani ameposti picha katika Instagram akiwa na 'asali' wake huyo wa moyo, iiwa na maelezo; 'Mr and Mrs Ozisto!, yaani Bwana na Bibi Ozisto.



Posh na Becks wapya: Mahusiano ya wawili hawa yanafananishwa na mahusiano na Waingereza hao enzi za ujana wao

Kifaa: Capristo amejipatia umaarufu nchini mwake kutokana na muziki, sasa akiwa anajitegemea baada ya kuanzia katika bendi ya wasichana watupu
Yeye na mpenzi wake huyo maarufu, wameteka vyombo vya habari London tangu wawasili katika Jiji hilo na hivi karibuni alinaswa akimpiga picha Capristo barabarani.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alimuambia mchezaji huyo mwishoni mwa msimu uliopita kwamba amezidisha tabia yake ya kujirusha, kitu ambacho kambi ya Ozil ilikanusha.
Ozil hakuwa katika ubora wake haswa kwenye mechi na Liverpool Jumamosi, lakini bado alitoa mchango katika mabao yaliyofungwa na Santi Cazorla na Aaron Ramsey, akiiwezesha Arsenal kujitanua kileleni kwa wastani wa pointi tano zaidi.
Sema chiizzz! Capristo akipozi kupigwa picha na Ozil 
Injini: Kiungo huyo wa Ujerumani aliichezea Arsenal ikiifunga Liverpool 2-0 Jumamosi Uwanja wa Emirates



.png)
0 comments:
Post a Comment