• HABARI MPYA

    Thursday, November 07, 2013

    DIDA ADHIHIRISHA YEYE KIPA KWELI, AIONGOZA YANGA MECHI NNE BILA KUFUNGWA HATA BAO MOJA

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    KIPA wa pili wa Yanga SC, Deogratius Munishi ‘Dida’ leo amedaka mechi ya nne mfululizo bila kuruhusu hata bao moja, tmu hiyo ikishinda 3-0 dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Dida sasa wazi anaweza kuendelea kudaka katika mechi zijazo, maana yake anaelekea kumpindua aliyekuwa kipa wa kwanza wa timu hiyo, Ally Mustafa ‘Barthez’.
    Yanga One; Dida katikati waliopiga magoti amedaka mechi nne Yanga SC bila kufungwa hata bao moja

    Dida alianza kudaka mechi na Rhino Rangers mwezi uliopita, Yanga ikishinda 3-0 baada ya kipa wa kwanza, Ally Mustafa ‘Barthez’ kuruhusu mabao matatu ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili na timu hiyo kulazimishwa sare ya 3-3 ikitoka kuongoza 3-0 dhidi ya mahasimu Simba SC, Oktoba 20, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Akadaka tena mechi zilizofuata, Yanga ikishinda tena 3-0 dhidi ya JKT Mgambo, 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na leo.
    Barthez alidaka mechi zote tisa za mwanzo za Ligi Kuu za Yanga na kufungwa mabao 11, yakiwemo matatu katika sare ya 3-3 na Simba SC.
    Dida alisajiliwa Yanga SC msimu huu, akitokea Azam FC kwa ajili ya kuwa kipa wa pili wa timu hiyo, baada ya kutemwa kwa Mghana, Yaw Berko.
    Dida na Barthez wamewahi kudaka pamoja Simba SC kama wasaidizi wa Juma Kaseja, kabla ya kila mmoja kuondoka kwa wakati wake akikimbia benchi.
    Lakini tayari kuna habari kwamba, Yanga SC inataka kumsajili Kaseja dirisha dogo, maana yake inaongeza changamoto katika nafasi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIDA ADHIHIRISHA YEYE KIPA KWELI, AIONGOZA YANGA MECHI NNE BILA KUFUNGWA HATA BAO MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top