• HABARI MPYA

    Sunday, November 03, 2013

    BREAKING NEWZZZZZ; JEMBE ANGETILE OSIAH MALABEJA ANG'OLEWA TFF, WAMBURA ANAKAIMU NAFASI YAKE

    Tutakumisi jembe letu; Angetile Osiah Malabeja amepewa likizo TFF hadi atakapomaliza mkataba wake mwezi ujao
    Na Mahmoud Zubeiry, Posta
    KIKAO cha kwanza cha Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana chini ya Rais, Jamal Emil Malinzi kimemuengua Katibu Mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah Malabeja.
    Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na Wajumbe wakaafiki, lakini wanamng’oa kistaarabu.
    Angetile amepewa likizo ya hadi atakapomaliza Mkataba wake mwezi ujao na kwa sasa, aliyekuwa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.
    Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
    Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.
    Jamal Malinzi
    Rais, Dar es Salaam
    Novemba 3, 2013
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWZZZZZ; JEMBE ANGETILE OSIAH MALABEJA ANG'OLEWA TFF, WAMBURA ANAKAIMU NAFASI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top