• HABARI MPYA

  Wednesday, July 04, 2018

  WERRASON AJA NCHINI KWA MAONYESHO MATATU, DAR, ARUSHA NA MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWANAMUZIKI nguli kutoka Jamhuri ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda, anatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.
  Mratibu wa ziara ya mwanamuziki huyo, Lengos VIP alisema kuwa mwanamuziki huyo nguli anawasili leo saa 4, asabuhi kwa ajili ya maonesho hayo maalum.
  Alisema kuwa Mwanamuziki huyo ataanza onyesho la kwanza mkoani Arusha siku ya Ijumaa ya Julai 6 na siku ya pili ya Julai 7, atakuwa mkoani Mwanza huku onyesho la mwisho litafanyika Mkoani Dar es Salaam.

  Werrason Ngiama Makanda anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya kufanya maonyesho Mwanza, Arusha na Dar es Salaam 

  Alisema mkoani Arusha Mwamuziki huyo atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Mjengoni Club, wakati Mwanza atafanya mambo yake kwenye ukumbi wa Rock City na Mkoa wa Dar es Salaam Life Park uliopo Mwenge (zamani Word Cinema).
  Werrason aliyeanzia katika bendi ya Wenge BCBG,  miongoni mwa wanamuziki wa Congo wanaopata nafasi za kupata mwaliko wa kuja kutoa burudani hapa nchini,  huku mratibu wa maonyesho hayo akiwataka mashabiki wajitokeze kupata burudani nzuri kutoka kwa nguli huyo.
  Mwanamuziki huyo amekuwa akifanya ziara katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania na kufanya vizuri kwa mashabiki kukubali ujio wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WERRASON AJA NCHINI KWA MAONYESHO MATATU, DAR, ARUSHA NA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top