• HABARI MPYA

  Wednesday, July 04, 2018

  KOCHA MEXIME ‘AKUNA KICHWA’ NAMNA YA KUZIBA PENGO LA JUMA KASEJA KAGERA SUGAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Kagera Sugar ya Bukoba, Mecky Mexime amesema kwamba atakuwa makini katika kuziba nafasi za wachezaji walioondoka baada ya msimu ili kuhakikisha anapata watu sahihi.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu, Mexime amesema kwamba wachezaji walioondoka kipa Juma Kaseja aliyehamia KMC, beki Mohammed Faki, kiungo Ally Nassor ‘Ufudu waliohamia JKT Ruvu za Dar es Salaam na mshambuliaji Jaffar Kibaya aliyehamia Mtibwa Sugar ya Morogoro wote walikuwa muhimu.
  Mexime amesema kwamba na kutokana na umuhimu wa wachezaji hao, analazimika kuwa mtulivu mno kuhakikisha anapata wachezaji mbadala watakaokwenda kuziba vyema nafasi za nyota hao walioondoka.
  Juma Kaseja (kushoto) amejiunga na KMC akitokea Kagera Sugar ya Bukoba 

  Mexime amesema kwamba kwa ujumla atakuwa makini mno katika kufanya zoezi la usajili kuhakikisha anaingiza wachezaji ambao watakwenda kuisaidia timu.
  Kagera Sugar ilimaliza Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika nafasi ya tisa baada ya kujikusanyia pointi 37 katika mechi 30 za msimu uliopita.
  Lakini Kagera Sugar zaidi inajivunia kuwa timu pekee iliyowafunga mabingwa, Simba SC 1-0 Mei 19 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam mbele ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, John Pombe Joseph Magufuli. Ni siku hiyo ambayo, Rais Magufuli aliwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MEXIME ‘AKUNA KICHWA’ NAMNA YA KUZIBA PENGO LA JUMA KASEJA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top