• HABARI MPYA

  Sunday, July 01, 2018

  URUSI YAING'OA KWA MATUTA HISPANIA KOMBE LA DUNIA

  Kipa wa Urusi, Igor Akinfeev akiokoa penalti ya kiungo wa Hispania, Koke na kuipa ushindi wa penalti 4-3 timu yake kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia leo Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow. Akinfeev aliokoa pia penalti ya Iago Aspas huku za Iniesta, Gerard Pique na Sergio Ramos zikimpita. Waliofunga penalti za Urusi ni  F. Smolov, Fyodor Ignashevich, Aleksandr Golovin na Denis Cheryshev na sasa Urusi wenyeji hao watakutana na mshindi kati ya Croatia na Denmark.
  Katika dakika 120 za mchezo huo, Hispania ilitangulia kwa bao la kujifunga la Sergey Ignashevich dakika ya 12, kabla ya Artem Dzyuba kuwasawazishia Urusi dakika ya 41 kufuatia Gerard Pique kuunawa mpira kwenye boksi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: URUSI YAING'OA KWA MATUTA HISPANIA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top