• HABARI MPYA

  Sunday, July 01, 2018

  RAYON SPORTS YALAZIMISHA SARE KWA GOR MAHIA KOMBE LA KAGAME

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  MCHANA wa leo Rayon Sports ya Rwanda ikicheza mchezo wa Kundi B katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, imelazimisha sare ya mabao 2-2.
  Katika mchezo huo uliochezwa kuanzia saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Gor Mahia ilitangulia kupata mabao mawili ambayo yalidumu hadi mapumziko.
  Gor Mahia ilipata bao la kwanza dakika ya 35 mfungaji akiwa ni Tuyisenge Jacques akimalizia pasi ya Guikan Ephrem. Bao la pili la Gor Mahia liligungwa dakika ya 41 na Mieno Humphrey akipokea pia pasi ya Guikan.

  Kipindi cha pili Rayon Sports ilizinduka na kufanya mashambulizi ya nguvu na kufanikiwa kupata bao la kwanza kwa njia ya penalti dakika ya 62 mfungaji akiwa ni Ismail Diarra. 
  Dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo huo, Rayon Sports ilipata napata bao la kusawazisha lililofungwa na Pierre Kwizera aliyewahi kuichezea Simba.
  Matokeo hayo yamelifanya Kundi B kuongozwa na AS Ports ya Djibouti ambayo jana jioni iliifunga Lydia Ludic ya Burundi mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex.
  Gor Mahia na Rayon ndizo zinazofuata halafu Lydia inashika mkia katika Kundi B. Keshokutwa Jumanne mechi nyingine za Kundi B zitachezwa ambapo Rayon itacheza na Ports huku Gor Mahia ikivaana na Lydia mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAYON SPORTS YALAZIMISHA SARE KWA GOR MAHIA KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top