• HABARI MPYA

  Tuesday, July 03, 2018

  TFF YAWAPONGEZA WADAU WA SOKA WATATU WALIOTEULIWA NA RAS DK MAGUFULI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amewapongeza wanamichezo watatu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kushika nyadhifa mbalimbali.
  Wanamichezo waliopata nafasi hizo ni Mussa Ramadhan Sima aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira, Athuman Kihamia aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi (NEC) na Ramadhan Kailima aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Rais wa TFF, Karia amesema kwa niaba ya TFF anawapongeza Wanamichezo hao kwa nafasi zao mpya walizoteuliwa anaamini kwa uchapakazi wao hawatamuangusha Rais John Pombe Magufuli.

  Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) amewapongeza wanamichezo watatu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kushika nyadhifa mbalimbali 

  “Kwa niaba ya TFF nawapongeza wanamichezo wenzetu Kihamia,Sima na Kailima kwa uteuzi wa nafasi zao mpya na nawatakia kila la heri kwenye nafasi zao”Alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.
  Kihamia yupo kwenye Kamati ya Ajira ya TFF wakati Sima ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira Wa Miguu Mkoa wa Singida.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWAPONGEZA WADAU WA SOKA WATATU WALIOTEULIWA NA RAS DK MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top