• HABARI MPYA

  Tuesday, July 03, 2018

  MFADHILI WA ZAMANI WA SIMBA SC, PROMOTA MAJI MAREFU AFARIKI DUNIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa mfadhili wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani (Profesa Maji Marefu), amefariki dunia usiku wa Jumatatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema Mbunge huyo amefariki akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, ICU alipokuwa amelazwa.
  Aligaesha amesema Profesa Maji Marefu amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu dhidi ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akimjulia hali Profesa Maji Marefu hivi karibuni 

  "Tulimpokea hapa Muhimbili akitokea Hospitali ya Kanda Dodoma Juni 20, mwaka huu, alilazwa wodi namba 18 katika jengo la  Sewahaji na baadae Juni 30 juni, mwaka huu alihamishiwa ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) ambako alilazwa hadi mauti yalipomkuta," amesema Aligaesha.
  Umaarufu wa Maji Marefu ulianzia kwenye uganga wa tiba za jadi kabla ya kuhamia kwenye michezo akijipambanua kama shabiki na mpenzi wa Simba SC ambayo alikuwa akiisaidia mara kwa mara miaka ya 1990 hadi 2000.
  Na ni wakati huo pia alikuwa promota wa ngumi za kulipwa akiandaa mapambano mbalimbali makubwa ya ngumi nchini kati ya Dar es Salaam, Tanga na Nairobi nchini Kenya.
  Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Profesa Maji Marefu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MFADHILI WA ZAMANI WA SIMBA SC, PROMOTA MAJI MAREFU AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top