• HABARI MPYA

  Thursday, July 05, 2018

  REFA OSMAN KAZI KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI JULAI 7 WASHINGTON

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  REFA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Osman Kazi ndiye atakayechezesha mechi ya soka baina ya wapenzi wa Simba na Yanga miongoni mwa Watanzania wanaoishi Marekani itakayofanyika Julai 7, mwaka huu mjini Washington DC.
  Akizungumza kwa simu kutoka Maryland, Marekani leo, Mratibu wa mchezo huo utakaokwenda sambamba na tamasha la kila mwaka la DMV Old School Reunion, Lucas Mkabu ‘Dj Luke’, amesema kwamba Kazi anatarajiwa kuwasili Washington Jumamosi wiki hii na atachezesha mechi hiyo akisaidiwa na marefa wa Marekani.
  “Marefa wasaidizi watatoka hapa haopa Marekani, na kwa ujumla maandalizi yanaendelea vizuri,”amesema na kuongeza kwamba jezi zitakazotumika katika mchezo huo, ambazo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Davis Mosha zimewasili jana.
  Osman Kazi (kulia) atachezesha pambalo la Simba na Yanga za Marekani Julai 7, mwaka huu mjini Washington DC 

  “Tunamshukuru sana Mosha kupitia kampuni yake ya Dellina ametupa udhamini wa vifaa vya michezo, yaani jezi za kisasa mpya ambazo zimekwishawasili na zitagawiwa kwa timu zote mbili kwa ajili ya mchezo huo,”amesema Dj Luke, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Tanzania waishio maeneo ya Washington DC, Maryland na Virginia uitwao DMV.
  Luke amesema mechi hiyo itaanza Saa 10:00 jioni kwa saa za Marekani na itafanyika Uwanja wa 830 Ridge Rd, SE Washington, DC 20019 na rekodi inaonyesha wapenzi wa Yanga wamekuwa wakiitambia Yanga.
  Amesema nyota wa Bongo Muvi, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ ni miongoni mastaa ambao wanatarajiwa kupambana burudani hizo ambazo zitapambwa na starehe, vyakula, vinywaji, Fasheni, Michezo na Nyama choma na atawsili Jumamosi.
  “Mona tayari yupo hapa Marekani, kwa sasa yupo Houston na atafika hapa Washington Jumamosi tayari kabisa kupamba tamasha hilo,”amesema.
  Kuanzia kesho, Julai 6 hadi 8 mambo yatakuwa Oxford Center, 9700 Martin L King Jr Hwy, Lanham, MD 20706 kabla ya kumalizia kwa disko la nguvu kuanzia Saa 3:00 usiku DMV International VIBE kwa kiingilio cha dola 50 ambacho kitaambatana na pfa ya kinywaji.
  Jumamosi ya Julai 7 kuaniza Saa 4:00 asubuhi litafanyika Bonanza la Basketball viwanja vya 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019 kabla ya mchezo wa Simba na Yanga kuchukua nafasi 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019.
  Na kuanzia Saa 3:00 usiku litaporomoshwa disko la nguvu la “Old School Reunion Party” ambalo halijawabui kutokea chini ya ma DJ wakali Amerika Kaskazini, Dj Luke Joe na Dj Dennis The Funkhouse na siku mambo yote gharama yake itakuwa dola 80 pamoja na chakula na vinywaji kutwa kucha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA OSMAN KAZI KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI JULAI 7 WASHINGTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top