• HABARI MPYA

  Thursday, July 05, 2018

  AZAM FC YAWAADHIBU WANAJESHI WA ZANZIBAR, VIPERS YAWANYANYASA KATOR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI za mwisho za Kundi A la michuano ya kombe la Kagame zimechezwa usiku wa leo katika viwanja viwili jijini Dar es Salaam.
  Kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, mabingwa watetezi Azam FC wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKU ya Zanzibar.
  Mabao ya Azam katika mchezo huo yalifungwa na Ditram Nchimbi na Frank Domayo na sasa katika msimamo wa Kundi A, Azam ipo kileleni ikiwa na pointi saba kifuatiwa na Vipers ya Uganda yenye pointi tano.

  Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa 1:00 usiku, Vipers ya Uganda imeifunga Kator FC ya Sudan Kusini mabao 3-0.
  Azam na Vipers tayari zimefuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Kageme lakini JKU yenye pointi nne inasubiri bahati ya kuvuka kama mshindwa bora.
  Kesho zitachezwa mechi za mwisho za Kundi B ambapo AS Ports ya Djibouti itacheza na Gor Mahia ya Kenya huku Lydia Ludic ya Burundi itacheza na Rayon Sports ya Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWAADHIBU WANAJESHI WA ZANZIBAR, VIPERS YAWANYANYASA KATOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top