• HABARI MPYA

  Tuesday, July 03, 2018

  RAYON YAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA KAGAME, YATOA SARE 1-1 NA WADJIBOUTI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MICHUANO ya Kombe la Kagame imeendelea leo mchana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Rayon Sports ya Rwanda imetoka sare ya bao 1-1 na AS Ports ya Djibouti.
  Katika mchezo huo wa Kundi B uliochezwa kuanzia saa 8:00 mchana, Pierre Kwizera ndiye aliyeifungia bao pekee la Rayon katika dakika ya 23 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Ports.
  Bao hilo la Kwizera aliyewahi kuchezea Simba lilidumu hadi mapumziko na katika kipindi cha pili Ports walicharuka na kucheza soka la kushambilia zaidi.
  Ports ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 83 mfungaji akiwa ni Mohdi Housein.

  Matokeo ya mchezo huo yameiweka Ports kileleni ikiwa na pointi nne ikifuatiwa na Rayon yenye pointi mbili baada ya kutoka sare katika mechi mbili.
  Katika mchezo wa kwanza wa Kundi B, Rayon ilitoka sare ya mabao 2-2 na Gor Mahia huku Ports ikiifunga Lydia Ludic ya Burundi mabao 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAYON YAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA KAGAME, YATOA SARE 1-1 NA WADJIBOUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top