• HABARI MPYA

  Friday, July 06, 2018

  PLUIJM: ILI UCHEZE AZAM FC CHINI YANGU, ONYESHA JUHUDI NA NIDHAMU

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya Mkuu wa Azam FC, Mholanzi Hans van der Pluijm amewataka wachezaji wa timu hiyo kuwa na nidhamu pamoja na kujituma ili waweze kupata nafasi ndani ya kikosi chini yake msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
  Kocha huyo aliyetoka Singida United na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Azam FC ameyasema hayo kwenye utambulisho wake uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano Mzizima.
  Kocha Hans amesema wachezaji anaowataka yeye ni wachezaji ambao wanajituma uwanjani na wenye nidhamu ya hali ya juu na chaguo lake yeye ni mchezaji mrefu lakini hata ukiwa mchezaji mfupi ukijituma na ukawa na nidhamu basi kwake utanikuwa ni mchezaji bora ndani ya kikosi chake.

  Hans van der Pluijm amewataka wachezaji wa Azam kujituma ili kupata chini yake 

  Hans ameongeza kuwa kitu kilichomsukuma mpaka kuingia mkataba na Azam FC  ni kutokana na uongozi wa Klabu hiyo kuwekeza kwa kila idara katika Klabu hiyo na anaamini kuwa kuwepo kwake ndani ya Timu hiyo itapata ubingwa msimu ujao. 
  Wakati huo huo Kocha huyo ameongeza kuwa sababu ya kumchagua Kocha Juma Mwambusi kuwa Kocha wake msaidizi ni kutokana na Kocha huyo kuwa Kocha mzuri na anaamini kwa kushirikiana nae watafanya vizuri ndani ya Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM: ILI UCHEZE AZAM FC CHINI YANGU, ONYESHA JUHUDI NA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top