• HABARI MPYA

  Friday, July 06, 2018

  PICHA ILIYOMTOA MACHOZI ATHUMANI CHINA, GWIJI WA SOKA YA TANZANIA

  "HII picha imenitoa sana machozi na inabidi nielekeze hisia na hasira zangu kwa serikali yetu ya mheshimiwa Doctor Magufuli na Waziri mwenye dhamana ya michezo.
  Picha hii inanitoa machozi kwa kuwa naiangalia safari yangu ya uchezaji ilipotokea hapa tena nikiwa mtoto uwezi sema hata ni kijana nipo na magwiji wa soka ambao walinilinda na kuniongoza kama mboni ya jicho kuakikisha nafikia malengo yangu ya kuwa mtu maharufu.
  Picha hii inanitoa machozi kuona nini mwisho wa umaarufu wangu utakapokua siku moja nitakapoanguka kitandani.
  Picha hii inanitoa machozi kuona wale wote waliokua wakinilinda kama mboni wakianza kuanguka mmoja baada ya mwingine pasipo taifa ambalo wamelitumia na kulifanya liwe na furaha aliwajali tena wala kuwathani hata chembe.
  Picha hii inanitoa machozi kuona mtu aliyekua akinipigania kwa hali na mali leo yupo kitandani na aoni tena kinachosikitisha hakina msaada wowote wa ki serikali
  Picha hii inanitoa machozi na kutaka fikisha ujumbe wangu kwa rais si kwamba Kila aliyekupigania au kukupa support basi ni lazima alikuja majukwaani na kupiga push-ups hapa na wewe tupo tuliokupa support kwa kuwaomba washabiki wetu wakupigie kula tukiamini ni rais utakae kuja kubadirisha mambo.
  Picha hii inanitoa machozi leo Mzee majuto Mzee mrema spika ndugai wastara wanapelekwa India kwa matibabu siyo Allan Shomari ambayo kwa miaka kadhaa yupo kitandani anasumbuliwa ugongwa wa kupofuka kwa macho
  Simanishi hawa wasanii awastahili msaada wa matibabu la hasha ninachomanisha kama wale wengine W amepata msaada wa matibabu toka serikali kuu basi ndugu yetu Allan’s Shomari anastahili naye kupatiwa msaada wa kimatibabu
  Picha hii imenitoa machozi kwa kuwa kuna msemo niounzisha mwenyewe kuwa kuzaliwa mchezaji mpira Tanzania ni Sawa na kulaanika naona sasa unajidhihirisha kwa watu Hawa walioleta furaha na faraja kwa mamilioni ya watanzania waliokua wakijazana Kila wiki kwenye viwanja vya mipira kuwapatia wananchi furaha na kuwatoa maumivu yao waliyokua wakiyapata kwa wiki nzima ya ujenzi wa taifa viwandani na mashambani leo mwisho wake hunakua hivi,".
  (Maelezo haya yameandikwa na Athumani China, kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyecheza klabu za Yanga na Simba za Dar es Salaam na Walsall FC ya England)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PICHA ILIYOMTOA MACHOZI ATHUMANI CHINA, GWIJI WA SOKA YA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top