• HABARI MPYA

    Friday, July 06, 2018

    CAVANI BADO SHAKANI KUIVAA UFARANSA LEO KOMBE LA DUNIA

    MSHAMBULIAJI Edinson Cavani bado yupo shakani kuichezea timu yake ya taifa, Uruguay mechi ya Robo Fainali Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa leo.
    Hiyo ni baada ya kocha Oscar Tabarez kushindwa kuelezea maendeleo ya mchezaji huyo kuelekea mchezo wa leo jioni.
    Cavani alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa Uruguay wa 2-1 dhidi ya Ureno hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia, kabla ya kusaidiwa na Cristiano Ronaldo kutoka nje kufuatia kuumia.
    Nyota huyo wa Paris Saint-Germain alifanya mazoezi peke yake jana kuelekea mchezo wa leo na Les Bleus mjini Nizhny Novgorod.

    Edinson Cavani bado yupo shakani kuichezea Uruguay dhidi ya Ufaransa leo 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAVANI BADO SHAKANI KUIVAA UFARANSA LEO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top