• HABARI MPYA

  Friday, July 06, 2018

  PIGO BRAZIL KUELEKEA MECHI NA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA LEO

  BEKI wa Brazil, Danilo hataweza kucheza mechi zilizosalia za Kombe la Dunia baada ya kuumia enka mazoezini.
  Shirikisho la Soka la Brazil limesema kwamba beki huyo wa kulia wa Manchester City aliumia enka ya mguu wake wa kushoto wakati wa mazoezi ya timu hiyo mjini Kazan jana, siku moja tu kabla ya Brazil kucheza na Ubelgiji katika mchezo wa Robo Fainali leo.
  Shirikisho limesema kwamba vipimo vimethibitisha mchezaji huyo hataweza kupona kwa wakati kuendelea kucheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.
  Lakini mchezaji huyo wa Manchester City atabakia kikosini hadi mwisho wa safari ya Brazil kwenye michuano hiyo.

  Danilo hataweza kucheza mechi zilizosalia za Kombe la Dunia baada ya kuumia enka mazoezini jana 

  Danilo aliichezea Brazil mechi ya ufunguzi dhidi ya Uswisi, lakini akakosekana kwenye mechi dhidi ya Costa Rica na Serbia kwa sababu ya maumivu ya nyonga ya kulia aliyoumia mazoezini pia.
  Akarejea katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Mexico kwenye hatua ya 16 Bora, lakini kocha Tite akamuanzisha mbadala wake, Fagner.
  Tite alisema beki wa kushoto, Marcelo aliyeuima mgongo kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Serbia, ataanza dhidi ya Ubelgiji leo baada ya kupona.
  Mshambuliaji Douglas Costa pia atakuwepo kwenye mchezo wa Robo Fainali baada ya kupona maumivu ya mshipa wa kulia wa pua yaliyomkosesha mechi dhidi ya Serbia and Mexico.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO BRAZIL KUELEKEA MECHI NA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top