• HABARI MPYA

  Friday, July 06, 2018

  KOCHA SIMBA SC ASEMA WADJIBOUTI WATAKUFA MAPEMA WATAKE WASITAKE

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KAIMU kocha Mkuu wa Simba SC, Mrundi Masoud Juma amesema kwamba ana uhakika wa kuibuka na ushindi dhidi ya AS Ports ya Djibouti katika mchezo wa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Jumapili.
  Simba watamenyana na Wadjibouti hao katika Robo Fainali Jumapili, siku ambayo na Gor Mahia ya Kenya itamenyana na Vipers ya Uganda, wakati Robo Fainali nyingine zitafuatia Jumatatu kati ya Azam FC na Rayon na Singida United na JKU. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online baada ya mazoezi ya asubuhi Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam leo, Masoud amesema kwamba Vipers ni timu nzuri lakini wataifunga.

  Masoud Juma (kushoto) amesema wataifunga AS Ports ya Djibouti Jumapili 

  "Nimepata nafasi ya kuwaona wakicheza ni timu nzuri inayocheza soka la kasi, lakini sisi tunatakiwa kuwa zaidi yao," amesema.
  Simba SC ilifanikiwa kwenda Robo Fainali baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi C mbele ya Singida kufuatia sare moja na kushinda mechi mbili.
  Ilizifunga Dahadaha ya Somalia 4-1 na APR ya Rwanda 2-1 katika mechi zake za mwanzo za Kundi C kabla ya kukwaa kisiki kwa Singida ya kocha Ahmed Morocco.
  Kwa sare hiyo, Simba SC ilimaliza na pointi saba, sawa na Singida United, lakini Wekundu wa Msimbazi wakamalizia juu kutokana na wastani wao mzuri wa mabao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA SIMBA SC ASEMA WADJIBOUTI WATAKUFA MAPEMA WATAKE WASITAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top