• HABARI MPYA

  Monday, July 16, 2018

  OKWI AREJEA KAZINI SIMBA SC BAADA YA MAPUMZIKO YA KUTOSHA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI nyota wa Simba Emmanuel Okwi amerejea nchini jana usiku tayari kuungana na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mapumziko ya tangu Mei.
  Okwi ambaye ni mume wa Florah Woods alikuwa kwao Uganda katika mapumziko marefu ya baada ya msimu na sasa ataungana na wachezaji wenzake kwa safari ya Uturuki kwenda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, Meneja wa Simba, Richard Robert amesema Okwi ameingia usiku wa jana na yuko tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya 
  Alisema mbali na Okwi pia mshambuliaji wao mwingine mpya, Meddie Kagere raia wa Rwanda mzaliwa wa Uganda, atarejea kesho baada ya kwenda kwao Jumamosi kuweka mambo yake sawa.

  Emmanuel Okwi (kulia) akiwa na Mbunge, Mussa Azzan 'Zungu' ambyae ni mpenzi mkubwa wa Simba SC
  "Okwi ameingia jana , Kagere atarejea kesho akitokea kwao alipokwenda kufuata vitu vyake kwa ajili ya kuja kuanza maisha mapya," alisema 
  Richard alisema  kikosi cha timu kinatarajia kuondoka wiki hii kwenda uturuki kwa ajili ya kambi 
  Simba inatarajia kuondoka Nchi ijumaa kuelea Nchini huko kwa kuweka kambi ya siku 18 na watarejea kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day. 
  Okwi amekuwa na mapumziko mazuri ya miezi miwili na nusu na ameposti picha na video kadhaa akiwa na mkewe, Florah kwenye vivutio mbalimbali nchini kwao, Uganda. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AREJEA KAZINI SIMBA SC BAADA YA MAPUMZIKO YA KUTOSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top